Wednesday, September 21, 2011

WABUNGE WA VITI MAALUMU RUDINI KWA WALIYO WACHAGUA,MSIKILIZE SHIDA ZAO

Blog hii imekutana na akina mama kadhaa wakiwalalamikia wabunge wa viti maalumu nchini kwa vitendo vyao vya kusahau kwenda kutoa shukurani kwa akina mama ambao wana matatizo kibao yanayo hitaji wawakilishi wao kuwa saidia,

Waheshimiwa wabunge wa viti maalumu tangu wachuguliwe na akinamama wa chama Tawala na wengine wamebahatika kupata vyeo vya juu kama uwaziri,ukuu wa mikoa.hawaja rudi kuwashukuru akina mama wenzao,akina mama hao waliwaamini kuwa watakuwa tayari kuwa wawakilishi na msaada mkubwa katika masuala ya maendeleo.
Wanasema wakitaka uongozi wanakaa  na akimama wenzao lakini wakishachaguliwa tu wanaondoka na kukaa Dar es salaam mpaka uchaguzi ujao,je huo ndiyo uwakilishi wa kweli,je watajuaje matatizo ya akinamama wenzao au watapataje mikopo kwa ajili ya biashara ndogo ndogo ? ni maswali mengi Blog hii imekutana nayo kutoka mitaani. katika Manispaa ya Songea.

No comments:

Post a Comment