Friday, September 30, 2011

RAIS KIKWETE AWATAKA WANANCHI WA IGUNGA WAACHANE NA VIONGOZI WENYE UROHO WA MADARAKA UBINAFSI WAKATI AKIZUNGIMZA NA TAIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JANA

 Rais wa Jamhuri ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete kama kawaida yake aliyojiwekea ya kuzungumza na wananchi kupitia vyombo vya habari kila mwisho wa mwezi jana,alisema mwezi uliyopita uliuwa na matukio mengi ya  kusikitisha,kama ajali ya meli Zanzibar na  matukio mengine ya ajali za barabarani.
 Aidha ame mshukuru Rais wa Baraza la Mapinduzi Dkt Shein na Makamu wake wote wawili katika kushughulikia maafa hayo maiti 203 zilipatikana na kuzikwa ambapo maiti 197  walizikwa eneo la tukio,5 Kenye na Mmoja Tanga nao walizikwa walikopatikana,Rais kaendelea kutoa pole na rambirambi kwa ndugu na jamaa walifikwa na msiba huo na Taifa kwa ujumla.
Pamoja na mambo mengini Rais aliwasihi watumiji wa vyombo vya moto kuwa makini katika kuvitumia,pia kawataa wananchi wa Wilaya ya Igunga kujitoeza kwa wingi atika kumchagua kiongozi wanao mtaka,wasirubuniwe na viongozi wapenda madaraka na wabinafsi.

No comments:

Post a Comment