Monday, April 29, 2013

WASTAAFU WA UTUMISHI WA UMMA WALALAMIKIA UCHELEWESHWAJI WA MALIPO YA PESHENI ZAO BADALA YA MIEZI MITATU KULIPWA FEDHA HIZO NA HUCHELEWESHWA HADI MIEZI MINNE - RUVUMA

 Bwana Rashid Holela akielezea jinsi malipo ya wastaafu yanavyocheleweshwa katika Benki ya NMB tawi la Songea.Alisema fedha walizo fika kuzichukua zilikuwa zilipwe mwezi wa tatu lakini hadi leo tarehe 29/4/2013 fedha hizo hazijaingizwa.
Wasomaji wa Blog hii picha hiyo ya Bw.Rashid siyo 'Action' hapana anasema kwa jaziba akionyesha wazee wezake waliyo kaa katika ukuta wa Benki ya NMB bila kujua hatima yao kuhusu pesa hizo.Akimwambia Ripota na Mwakilishi wa Radio UHURU Mkoa wa Ruvuma Bwana Juma Nyumayo, kuwa waambie na wazee wengine wanakoisikia Radio hiyo kuwa wawaunge mkono maana kilio hicho wanaamini ni cha wengi ' aliyeshiba hamjui mwenye njaa' alisema Bw.Rashid.
 Bwana Rashid anasisitiza kuwa Serikali haiwatendei haki wazee waliofanya kazi serikalini wakiwa watumishi wa Umma. kwanza fedha tunazolipwa hazikidhi haja kutokana na maisha yalivyo kuwa magumu,pili pamoja na hicho kidogo kulipwa mapema, nacho kinacheleweshwa. Hivyo wanavyo fanya hivi hawaji kustaafu siku moja ? aliuliza Bw.Rashid.( Picha na Juma Nyumayo)
 Hapa Bw.Holela akimwita mzee mwenzake Bw. Mapunda afike apige picha pamoja ili kilio hicho kisiwe chake peke yake,wakati walikuwa pamoja wakiahangaika wapi wapate fedha,maana za Pesheni wenye zao wamegoma kuwapa.
 Huyo aliyesimama mwenye koti ndiye Mzee Tobiasi Mapunda kutoka Lituhi kuja Tawi la NMB Songea kufuatia Pesheni yake na kuambulia patupu.
Pamoja na kuwa na mwenzake Mzee mapunda lakini Bwana Holela Rashidi bado alikuwa akiendelea kulaumu utaratibu uliyo wekwa na Serikali wa kuwalipa Pesheni wastaafu kila baada ya miezi mitatu na kisha kupitiliza hadi miezi mnne.


WASTAAFU wa utumishi wa Umma katika Mkoa wa Ruvuma ,wanaulalamikia utaratibu wa malipo yao ya  Pesheni yanavyolipwa ambayo  hayaende kama serikali ilivyo tamka ya kulipwa kila baada  ya miezi mitatu mitatu.

Wakizungumza na Blog hii leo katika Manspaa ya Songea katika Tawi la Benki ya NMB walipo fika kuchukua fedha zao za mpesheni hawakuyaamini macho yao baada ya kukuta salio lao halitoshi.

Bwana Holela Rashidi anasema “ mpaka leo hii ni mwezi wa nne sasa hawajatuingizi fedha zetu za Pesheni ambazo zilitakiwa tuzichukue mwezi wa tatu, walituambia kuwa watakuwa wanatulipa kila baada ya miezi mitatu mitatu, lakini cha ajabu tunakwenda kwenye ITM kuangalia salio hakuna kilicho ingizwa.”

“Tumiitumikia nchi hii, leo serikali inatufanyia vitendo hivi, mbona ni manyanyaso makubwa  sana, wengine wanatoka mbali wilaya ya Mbinga kuja kufuata mafao yao na wanapoyakosa inawalazimu kukaa kwa jamaa zao, ambapo huleta kero kwa wenyeji wao” Alisema Bw.Rashidi.

Naye Mzee Tobias Mapunda ametoka Wilaya ya Mbinga,” anasema nimetoka Litui Wilaya ya Mbinga kuja kuchukua pesheni yangu ya miezi mitatu kama serikali ilivyo tuhaidi,lakini nilivyo angalia salio sikukuta fedha iliyoingizwa.na leo ni tarehe 29 mwezi wa nne, na fedhi hiyo ilibidi tulipwe tarehe 30 mwezi wa tatu”.

Aidha alisema kuwa tulienda hazina ndogo ya Mkoa wa Ruvuma ,na huko tuliambiwa fedha imishapelekwa Benki ya NMB Tawi la  Songea, lakini tulivyo fika kwa meneja wa Benki tawi hilo tuliambiwa fedha hazija fika, sasa tumlaumu nani ? kati ya Hazina na Benki? Huo ndiyo utaratibu wa serikali au ni utaratibu wa Hazina na Benki kuwaingiza Wastaafu katika madeni wasiyoyapanga ? aliuliza mzee Mapunda kwa uchungu mkubwa.

Hicho ndicho kilio cha wazee wa Utumishi wa Umma waliostaafu na walilitumikia taifa hili na kuliacha na watumishi wengine ambao na wao kuna siku watakuwa wastaafu kama walivyo wazee hao  Hivyo waliopewa dhama hiyo ya kuwatendea haki wazee hao wawahudumie wazee hao, sio wa mkoa wa Ruvuma peke yao, bali ugonjwa huu upo kwa nchi nzima, la kuwabeza wazee,lakini wanasahau kuwa na wao ni wazee wa baadaye.

No comments:

Post a Comment