Monday, April 22, 2013

BEAKING NEWSSSSSSSSSSSS: KUFUKUZWA BUNGENI NA KUJIUZURU KWA WAZIRI WA ELIMU KUNA UHUSIANO GANI ? BAADHI YA WABUNGE WALIYOFUKUZWA BUNGENI KWA UTOVU WA NIDHAMU WANADAI KWANINI WAZIRI WA ELIMU HAJIUZURU.

Watanzania tufike mahali tuseme, kuwa kuwepo na vigezo ambavyo vitasaidia kumpata mwakilishi wa jimbo lao Bungeni ambaye ni mwadilifu, sio tu anajua kuwashawishi wapiga kura wake na kisha akachaguliwa baadaye akawa kituko Bungeni.

Kuna msemo kuwa zamani watu walikuwa wakishindwa kuhoji mambo na wasomi walikuwa wachache na wale wachache walishindwa kuhoji kwa kuwa waliogopa kutia kitumbua chao mchanga,ni hoja yenye maantiki,Je sasa wasomi wengi wanye kisomo cha juu na wenye kujua kuhoji, kumekuwa na tofauti gani ya mwanzo wasomi wachache na waliogopa kuhoji na sasa wasomi wengi wanahoji mambo mengi kimaendeleo na heshima Bungeni?.

Utovu wa nidhamu ndani ya Bunge letu kumefanya baadhi ya Waheshimiwa wa bunge wakae nje ya Bunge kwa siku kadhaa.sasa cha ajabu wabunge hao wanamadi mengi kimsingi hayana uhusiano na kufukuzwa kwao.

Mf.Mbunge mmoja anadai kwanini waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Dkt Shukuru kawambwa hajiuzuru,hivyo Waziri huyo ndiyo aliyewaambia wakosenidhamu wakati wa majadiliaano ndani ya Bunge.Mbona wanapenda kumwandama waziri huyo bila sababu.

Hivyo Waziri huyo ndiyo alikuwa na wanafunzi siku ya kufanya mitihani na kuwaambia wachore picha kwenye karatasi za majibu au kutukana matusi ama kuandika  mistari ya Rap kiasi cha Album nzima,chonde tumrudie Mungu.

Dkt Kawambwa wakati shule utitiri za Sekondari za Kata zikijengwa nchini ndiye alikuwa Waziri wa Wizara hiyo, kwa nini  wasiwahoji waliyokuwa katika Wizara hiyo kuwa kwanini walianzisha sekondari zisizo na walimu, maabara, nyumba za walimu, majengo ya utwawala, vitabu vya kufundishia na kujifunzia na kama yote hayatoshi, Madai ya walimu yalianza kipindi hicho hicho  na yeye amekabidhiwa tu.

Chamsingi hapa tujitafiti tuone tumekosea wapi katika Elimu Nchini na siyo kujiudhuru  kwa Waziri Kawambwa ,kwa mtindo huo watajiuzuru wengi katika Wizara hiyo maana inachangamoto kibao,kisha ni kubwa mmno.

No comments:

Post a Comment