Thursday, April 25, 2013

HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA KULIPIA ADA YA MWAKA MOJA KWA WANAFUNZI WATATU WALOFANYA VIZURI MITIHANI YAO MWAKA JANA DARASA LA ZABA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Songea Bw.Nachoa Zatcharia  akielezea hali ya elimu ilivyo katika manispaa hiyo kwenye kikao cha Tathimini ya elimu mwaka 2013 ,kilicho fanyika katika ukumbi wa Songea Club leo.
Amesema kuwa pamoja na kuongoza kwenye matokeo kimkoa lakini bado changamoto bado zipo ni lazima zijadiliwe kwa makini na wadau wa elimu ili kuinua taaluma katika manispaa hiyo,Na kwamba wanafunzi watatu waliofanya vizuri katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi ,Manispaa hiyo itawalipia ada ya bweni ya sh.70,000/= kila mmoja kwa mwaka mmoja,
Wanafunzi hao ni pamoja na Sunday Msinza kutoka shule ya msingi Majimaji aliyepata alama 215 kuchaguliwa Mzumbe wa pili ni Ayoub Cosmas Ilomo aliyepata alama 213 na kwenda Kibaha na watatu Msichana Genoveva  Ndunguru  aliyepata alama 202 na kwenda Msalato.
 Afisa elimu Taaluma wa manispaa hiyo Bi.Consesa Mbena Kisoma taarifa ya elimu ya Manispaa hiyo
 Baadhi ya wadau wa elimu
Afiesa Elimu wa Manispaa hiyo Bi.Edith Matata Kagomba

No comments:

Post a Comment