Tuesday, April 23, 2013

RAIS UHURU KENYATTA ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI LENYE MAWAZIRI 18, KATI YA HAO AMETANGAZA WANNE NA WENGINE WATAENDELEA KUTANGAZWA.

 Rais Uhuru Kenyatta ametangaza Baraza la mawaziri lenye Wizaza 18.Ameanza kutangaza Wizara nne,ambapo amemtangaza Dkt.Fredy Matiang'a.Waziri wa Habari ,Mawasiliano na Teknolojia ( ITC) Ministry of Information ,Communication and Technology, aliye simama kulia kwake.
 Wapili ni Bw. Henry Rotich waziri wa Fedha (Ministry of National Treasury )
 Watatu alikuwa Bw.James Wainaina Masharia Waziri wa Afya ,( Ministry of Health}
 Na wanne alikuwa Balozi Amina Mohamedi Mwanasheria  Ministry of Foreign Affairs
 Waandishi wa habari ambao walikuwa wakirusha kipindi hicho live ni Source wa Blog hii
Ni waandishi wa kutoka vyombo mbalimbali wakiwa katika viwanja vya Ikulu ya Kenya wakati Baraza la mawaziri likitangazwa.


RAIS Uhuru Kenyatta na Makamu wake Willium Rutto leo wametangaza Baraza jipya la Mawaziri,Lakini kati ya hao, Rais Uhuru Kenyatta ametangaza mawaziri wanne ambao si wanasiasa.Ni tukio la kistoria kufanyika nchini Kenya.

Rais aliwataja Mawaziri hao kuwa ni pamoja na :-
  • Dkt. Fredy Okengo Matiangi Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ( ITC ).Ministry of  Information, Communication and Technology ( ITC )
  • Henry Rotich Waziri wa Fedha ( Ministry of National Treasury )
  •  James Wainaina Masharia  Waziri wa Afya ( Ministry of Health )
  • Balozi Amina Mohamed Ministry of Foreign Affairs

Alisema majina mengine yataendelea kutangazwa ,na kwamba kazi itaanza mara moja kuaznia kesho.Alisema Kenya ina wasomi wengi na wataalamu wengi lakini Katiba ya Jubilee imeweka kikomo cha kuchagua baraza la mawaziri kwa lengo la kupata baraza dogo ,ambalo lilisizidi wizara 22.
Kwa kutokana na wizara nne zilizotangazwa kutabakia na wizara 14 ambazo zitaendelea kueleweka hapo baadaye.
Kamati ya Bunge itawachunguza mawaziri hao na wengine kuona kwamba watalisaidia taifa la Kenya na watu wake katika kusukuma mbele maendeleo.
Rais Uhuru Kenyatta na Makamu wa kwake Willium Rutto walifika mbele ya waandishi wa habari bila Wapambe wao wakiwa  wamevalia mashati meupe na tai nyekundu bila makoti

No comments:

Post a Comment