Saturday, April 20, 2013

MKUU WA WILYA YA NACHINGWEA BI. REGINA CHONJO AAGIZA WAENDESHA BODABODA KUPATA LISENI YA UDEREVA WA PIKIPIKI

Mkuu wa Wilaya ya Nachingewa Mkoani Lindi Bi.Regina Chonjo amewaagiza waendesha bodaboda wa Wilaya hiyo kupata liseni ya kuendesha pikipiki,ili kupunguza ajali zinazotokea wanapowakimbia askari wa usalama barabarani kwa kuwa hawana liseni.
Bi.Chonjo alisema bodaboda ni kazi,hiyo ili wafanye kazi hiyo kwa umakini ni lazima kila mmoja wao apate liseni.
Alisema hayo wakati akiongea na waendesha bodaboda hizo mjini Nachingwea,na kwamba waendesha bodaboda hao wameshapata mafunzo ya usalama barabarani na hivyo itakuwa ni rahisi kwao kupewa liseni.( Source ITV )

No comments:

Post a Comment