Friday, April 19, 2013

CHAMA CHA MPIRA WA MIGUU KWA WANAWAKE ( TWFA) MKOANI RUVUMA WAKUFUNZI WA SOKA WATOE MAFUNZO YA KUTOSHA KWA MAKOCHA WANAWAKE

Mji wa Songea


CHAMA cha mpira wa miguu cha wanawakeTWFA mkoa wa Ruvuma kimewataka wakufunzi wa soka hilo watoe  mafunzo ya awali kwa makocha wanawake  ili waweze kuendeleza mchezo katika wilaya zote mkoani hapa.

   Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana Katibu wa TWFA mkoa, Inviolata Lwena alisema kuwa bado kumekuwa na tatizo la kuwapata wakufunzi kuendesha kozi ya awali ya makocha wanawake mkoani hapa

  Alisema katika kipindi cha hivi karibuni mwaka huu TWFA kupitia ofisi ya ofisa michezo, utamaduni na maendeleo ya vijana mkoa waliweza kuwateua wadau wawili kuhudhuria kozi ya program ya Tackla Africa Thoraht 11 mradi wa michezo shirikishi kwa jamii ambayo iliendeshwa na Baraza la michezo la Taifa BMT jijini Dar es Salaam.

    Akifafanua alisema wadau hao baada ya kurejea wameshindwa kuendesha kozi hiyo kama walivyoangizwa kabla ya kuondoka na badala yake wamekuwa wakigeuza mafunzo hayo waliyoyapata kama moja ya mradi bila ya kuwashirikisha viongozi wa TWFA ambapo alidai ni kinyume na sera ya Serikali ya kuendeleza michezo kwa jamii

    Aliwataja wadau hao ambao wamegeuza mafunzo hayo waliyoyapata kama mradi wao binafsi kuwa Mary Kapinga na Juma Mpogoro na kuwaacha wenzao wa TWFA wakiangaika kutafuta wakufunzi wa kuweza kutoa mafunzo ya awali ya ukocha kwa wanawake 20 ambao tayari alidai wamedhibitisha kuhudhuria kozi hiyo.

    Alisema hatua iliyofikiwa na wadau hao wawili Kapinga na mwenzake  Mpogoro ya kukumbatia ujuzi waliupata na kushindwa kuwaendeleza wenzao wamekuwa wakichangia kudidimiza michezo na amewakata viongozi wa BMT iwajukulie hatua kali za kinidhamu ili tabia hiyo isiwaambukize wengine na kubakia kuua michezo.

    Hata hivyo alivyotafutwa Mary Kapinga kupitia simu yake ya kiganjani wenye namba 0763884810 hakuweza kupatikana kwani simu yake ilikuwa imefungwa muda wote na kushindwa kupata mawasiliano yake juu ya tuhuma hiyo inayomkabili.

    Naye Ofisa michezo utamaduni na maendeleo ya vijana mkoa, Hassan Katuli alipoulizwa alikiri kwa wadau hao kuhudhuria kozi ya kocha wa mpira wa wanawake na kuikalia bila ya kutoa mafunzo kwa wenzao kama walivyokuwa wameagizwa BMT ( source  Mhaiki Andrew, Songea )

No comments:

Post a Comment