Thursday, April 25, 2013

MKUU WA WILAYA YA SONGEA AWATAKA WENYE MADARAKA KUFANYA KAZI ZAO KWA UFASAHA,WALIMU WAFANYE KAZI ZAO WAKIZINGATIA KANUNI,ILI KUINUA TAALUMA

 Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Joseph Joseph Mkirikiti aliyekuwa Megeni rasmi katika kutathimini elimu katika Manispaa ya Songea leo.Bw.Mkirikiti alisema kila mmoja aliyepewa mamlaka katika Manispaa hiyo lazima atekeleze wajibu wake ipasavyo.
Aidha alisema kuwa kwenye mambo magumu wasifanye kuwa rahisi hasa katika kuinua taaluma katika Manispaa hiyo.Walimu wawajibike ipasavyo katika kufundisha,wasimamie watoto,wafundishe kwa upendo.
Kamati za shule na Bodi za shule ziwajibike kwa wanafunzi na wazazi katika uhamasishaji wa maendeleo ya elimu.
Alisema kuwa madiwani wote wafanye kazi kwa bidii bila kujali itikadi zao,kwa hiyo kamati za shule,bodi za shule wenyeviti wa serikali za mitaa na walimu wakifanya kazi zao kwa ufanisi matokeo mazuri yataonekana.
h
 Afisaelimu wa sekondari Manispaa ya Songea Bw.Leo L. Mapunda

 Mkuu wa Wilaya Bw.Joseph Joseph Mkirikiti kulia na Mkurugenzi wa Manispaa ya Songea Bw.Nachoa Zacharia
 Waheshimiwa madiwani
 Baadhi ya wadau wa elimu
 Waheshimiwa madiwani
Naibu Mstahiki Meya Wilon Kapinga akifunga mkutano huo,na kuagiza kwa wadau wa elimu kwenda kuyafanyia kazi maazimio yote yaliyo jadiliwa katika tathimini hiyo.Na kwamba kila mtu akatekeleze majukumu yake katika eneo lake la kazi.

No comments:

Post a Comment