Bei ya mchele katika maduka ya Manispaa ya Songea imeshuka kutoka sh.2,400/= hadi sh.1.600/= na 1.400/= kwa kilo moja ,hiyo imebainika katika duka moja la Matarawe Manispaa ya Songea lijulikanalo kana duka la Moyo kuwa wanauza mchele huo kwa bei aliyoitangaza Waziri Mkuu kwa wafanya biashara wa vyakula Jijini Dar es Salaam wauze mchele kwa bei ya sh.1,600/= wakati akipokea tani kadhaa za mchele kutoka nje.
Bw.Moyo alisema mchele unaokobolewa mashineni ni wa Tunduru,ambao bei yake ni nafuu ukilinganisha na mchele kutoka Kyela Mbeya bei yake imebakia palepale ya sh.2,400/=,2,500/= kwa ajili ya gharama za usafirishaji kutoka Kyela Mbeya hadi Songea.

No comments:
Post a Comment