Monday, April 15, 2013

RAI IMETOLEWA KWA WATANZANIA KUACHA SAKATA LA UCHINJAJI WA NYAMA KWA AJILI YA KITOWEO

 Mwenyeliti wa Makampuni ya IPP Dkt Reginald Mengi akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam,kuhusu tatizo linalojitokeza la kutaka kujua nani mwenye haki ya kuchinja/
Mfano wa sakata la madai ya uchinjaji katika mji mdogo wa Tunduma lilivyojitokeza hivi karibuni kama vurugu hizo zilizojitokeza katika sakata la uchinjaji katika mji huo Mkoani Mbeya.


RAI IMETOLEWA KWA WATANZANIA KUACHA SAKATA LA UCHINJAJI   ZAMANI WALIOKUWA  WAKICHINJA ILITAMBULIKA KUWA NI WAISLAM

IMETOLEWA Rai kwa Wanzania kuacha sakata la uchinjaji wa nyama ambayo hutumika na jamiinzima kwa ajili ya kitoweo,ambapo hapo awali waliyokuwa wakichinja nyama kwa ajili ya jamii walikuwa Waislamu.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP Dkt.Reginald Mengi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa tangu zamani uchinjaji ulikuwepo katika jamii ya Tanzania ,lakini hakukuwepo na malumbano haya yanayojitokeza hivi sasa,na kwamba jamii ikuwa ikitabua kuwa Waislamu ndiyo walikuwa wachinjaji wa kitoweo kitakacho tumika katika Jamii nzima.
Aidha alisema hajakataza watu wanaojichinjia kuku,mbuzi wao majumbani kwao kwa ajili ya matumizi ya familia zao,bali ni uchinjaji unao tumika na jamii nzima.

No comments:

Post a Comment