Friday, May 3, 2013

LEO NI SIKU YA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI, LAKINI UHURU HUO WA VYOMBO HIVYO UPO, NA WANAOFANYA KAZI KATIKA VYOMBO HIVYO WANAO UHURU HUO TUNAO USHUHUDIA LEO ?,BASI MIE NILIPITA MITAA YA MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA KAMA HIVYO

 Huu ni mmoja wa mtaa maarufu sana katika Manispaa ya Songea ,ambao leo siku ya Uhuru wa vyombo vya habari,Blog hii ilipitia,lakini palitulia sana,Wasomi wa Chuo kikuu cha Misheni walikuwa wakibukua kama kawaida yao.Aidha wafanya biashara wa maduka nao walikuwa wanaendelea.Nilijiuliza mbona watu wanaendelea kama vile hakuna tukio lolote.
 Lakini baadaye nilipata jibu kuwa Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari ni kitu wanaokifahamu wenye vyombo hivyo pengine na baadhi ya wanaofanya kazi katika vyombo hivyo.Inawezekana hata Serikali hazijui kitu hiki,wala hata viongozi hawaoni umuhimu wa kitu hicho.Inafurahisha ni sawa na baadhi ya watu wanasema hawali nyama ya mbuzi ili mchuzi wake nitajaribu kunywa.sasa ule mchuzi umetokana na kitu gani.
Tanzania tumeshuhudia waandishi wa habari wanavyofanya kazi katika mazingira magumu,wengine wanapoteza maisha yao kwa ajili ya kuisemea jamii,Ndugu yetu Mpendwa Marehemu David Mwangosi Iringa alikufa kifo kibaya hata watoto na jamaa zake wakaribu hawata kisahau.Je huo ndiyo uhuru wenyewe wa vyombo vya habari.
Kinacho shangaza Serikali na Jamii inawaona waandishi waandishi wa habari kama adui,lakini wanapotaka kufanikisha majambo yao wanawatafuta haohao maadui, wakifanikiwa hawana thamani nao tena,kwa mwenendo huo tutakuwa na uhuru wa kweli wa vyombo vya habari nchini na nje ya nchi?
Sindiyo Uhuru huo wa vyombo vya habari leo na hali ndiyo hiyo Manispaa ya Mji wa Songea kupitia Chuo kikuu cha Songea kuelekea kanisani hadi Majengo.Hiyo ndiyo siku niliyoitumia katika manispaa hii.
Ukweli vyombo vya habari bado vinakazi kubwa, mpaka vitambulike na vyenyewe kuwa vinakuwa na siku rasmi na viongozi wa wa serikali na wanachi wafike kusikia vilio vyao,na vikasikilizwa.Na siyo kama kilio cha samaki machozi yakaenda na maji.( I wish you all the best Media houses , News Organizations and my collage Journalists, to celebrate well in the media day.}

No comments:

Post a Comment