Saturday, May 11, 2013

WANACHUO SITA ( 6 ) WAHITIMU KOZI YA MIEZI 9 YA USHIRIKA NA SACCOS KATIKA CHUO CHA USHIRIKA SONGEA TAWI LA CHUO KIKUU CHA USHIRIKA MOSHI MJINI SONGEA

 Mgeni Rasmi na Afisa Ushirika wa Mkoa wa Ruvuma na Kaimu RAS Bw.Watson Nganiwa mwenye kaunda suti nyeusi akimpa cheti Mmoja wa wahitimu wa ' Professional Fanancial Cooperative Programme ( PFCMP} ya miezi 9 katika Chuo Cha Ushirika Songea Tawi La Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi Tanzania chenye matawi yake nchi nzima.
 Huyo ni Mhtimu wa Pili aliyepewa cheti ambapo waliopata vyeti ni sita wanaume watatu na wanawake watatu Mwenye suti na tai ndiye Mratibu wa Kituo cha Chuo cha Ushirika Songea Bw.Abel Raphael Ngowi
Mwenye suti nyeukundu naye ametunukiwa cheti,akiwa ni mfanyakazi katika chuo hicho Dada Lucida Chowo.
 Akina mama hawako mbele katika elimu ya Ushirika Huyo ni Bi.Tabasamu Adima Mbawala akionyesha cheti chake baada ya kukabidhiwa
 Bi fausta Kasuga mwenye nguo nyekundu ambaye ndiye Mratibu wa Mafunzo na mwalimu katika Chuo hicho na Afisa Ushirika wa Manispaa ya Songea akimpa mkono wa pongezi mwenyekiti za mafunzo hayo pia ni mhitimu Bw.Wanter Ndimbo baada ya kupewa cheti
Mwenyekiti Bw.Ndimbo akisoma risala mbele ya mgeni rasmi hayumo katika picha. Matukio mengine yataendelea kutolewa zaidi ili kukielewa vizuri chuo hiki.



WANACHUO sita wa ( course ya  Financial cooperative Programme ( PFCMP ) wakiwemo wanaume watatu na wanawake watatu wametunukiwa vyeti baada ya kusoma kwa miezi tisa katika Chuo Cha Ushirika Songea.katika Kozi ya Professional Financial Cooperative Management Programme (PFCMP)

Afisa Ushirika wa Mkoa wa Ruvuma ,pia na kaimu RAS wa mkoa wa Ruvuma Bw.Watson Nganiwa amewakabishi vyeti Bw. Kevin Ponera wa SACCOS Mshangano,Wanter Ndimbo SACCOS Walimu Vijijini, Pia mwenye kiti wa Mafunzo, Bi.Tamasamu Adimu Mbawala, Bw.Theophord Seif,Bi Lucida Chowo.

Aidha Bw. Nganiwa amesema elimu ndiyo  kila kitu katika maisha ya mwanadamu,na kwamba elimu haijali umri wa mtu.Na amweaasa wahitimu hao kuwa wawe  mabalozi wazuri huko wanakokwenda kwa kukitangaza chuo cha ushirika Songea Tawi la Chuo kikuu cha Ushirika Moshi kuwa kinatoa mafunzo kupitia elimu masafa.

Alisema wale wenye matatizo ya ada wafike kweke atazame namna ya kuwasidia ili watimize ndoto zao za kupaya elimu ya usimamizi wa Ushirika na SACCOS.katika SACCOS zao.

Awali Mratibu wa Chuo Kikuu hicho Bw. Abel Raphael Ngowi,amewapongeza wahitimu hao kwa kuweza kuhudhuria masomo kwa miezi 9 bila kutoa  kwa sababu zakushindwa kuhudhuria masomo, alisema masomo ya utu uzima siyo mchezo inatakiwa kujituma,na hivyo amewapongeza kwa kuhitimu kwao.ili wawe chachu kwa wengine wenye nia ya kusoma kupitia Elimu Masafa.

Alisema kwa kupata cheti peke yake bila kuonesha mabadiliko huko wanakokwenda itakuwa ni kazi bure, hata sifa za chuo hicho zitakuwa hazipo, alicho taka kwa wahitimu hao ni kuonyesha badaliko tofauti kabla hawajapata elimu ya Ushirika.na baada ya kupata taaluma hiyo katika SACCOS zao.

Bw.Ngowi alisema chuo hicho kinaendesha kozi za masafa ,ambapo kuna walimu wawili wanafundisha katika chuo hicho, aliwataja walimu hao kuwa ni pamoja na Bi.Fausta M. Kasuga,Mratibu wa Mafunzo pia ni Afisa Ushirika wa Manispaa ya Songea na Bw. Fredrick P. Kandosa

Ambapo Mratibu Msaidizi Bibi Benigna Nchimbi( Mrs Haule ), amewasihi wahitimu hao kuwa wakatumie vyema elimu waliyoipata, kisha kwa wale ambao watajiunga na masomo hayo, SACCOS zao zitoe ada ya kusomesha wasimamizi wa SACCOS hizo.

No comments:

Post a Comment