Askofu Mstaafu Norbet Mtega akihojiwa na Vyombo vya habari kuhusu uamuzi wa Kustaafu kazi za utume wake kabla ya miaka 75 ambayo Askofu anatakiwa kuomba kustaafu.
Ni picha ya Pamoja ya Mwandishi wa habari wa TBC Bw.Gerson Msigwa na Askofu Mtega
Mahojiano na waandishi wa habari
Picha ya pamoja na waandishi wa habari katika Bustani ya nyumba ya Uaskofuni Mjini Songea leo.
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja na Mhashamu Askofu Mtega
Askofu Mtega akiwa na mtangazaji wa Radio Maria Mbinga Bw. Nilai wa kushoto na Mwandishi wa habari mpiga picha Bw. Ndolanga na Nyuma yake Askofu ni Bibi Joyce Joliga mwandishi wa habari Gazeti la MwananchiNi picha ya Pamoja ya Mwandishi wa habari wa TBC Bw.Gerson Msigwa na Askofu Mtega
Kauli hiyo ameitoa leo mbele ya vyombo
vya habari alipokuwa akiongea navyo katika bustani ya nyumba ya uaskofuni
katika kanisa kuu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba la Mjini Songea.
Askofu Mtega alisema ni vyema kuacha
mapema kazi wakati mtu akiwa na nguvu,akili kuliko kusubili mpaka akili ichoke
kwa kusahau mambo.
Alisema ameomba kustaafu kabla ya miaka
ya kustaafu kwa maaskofu wa miaka 75.kutokana na matatizo ya kiafya ,mara
nyingine anasumbuliwa na BP.
Askofu Mtega amefanya utume wake kwa
miaka 28 ambapo Mkoani Iringa ametumikia kwa miaka 6 na Jimbo Kuu la Songea
ametumikia miaka 22, na kutoa huduma za kiroho na za kijamii zikiwemo za Elimu
,Afya pamoja na Mazingira.
Amesema kuwa yeye bado ni Askofu na
atafanya kazi zote atakazo ambiwa kufanya na Askofu Mkuu atakayeteuliwa, ambapo
kwa sasa anashikilia Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania, Mhashamu
Ngalalimnamtwa wa Iringa.
Amewashukuru waumini wote kwa
ushirikiano mwema waliouonyesha wakati wa utume wake,na amekuwa nao kwa moyo mmoja bila kukwaruzana
wala kugombana, aidha ameomba ushirikiani uimarike na kufanya kazi bila
kuingiza ukabila maana masuala ya ukabila yilipitwa na wakati.
No comments:
Post a Comment