Friday, May 10, 2013

WANANCHI WA KATA YA MAJENGO MANISPAA YA SONGEA WAILALAMIKIA MANSIPAA HIYO KUACHA KUSOMBA TAKATAKA HIZO KWA MUDA MREFU

 Hizo ni takataka zilizo zagaa kutoka mbele kwenyeGuma lililojegwa kwa ajili ya kukusanyia takataka.
Mbele ni duka la madawa nyuma na takataka kama zinavuonekana,hapohapo kunajiwe na Bendera ya Chama Tawala,

Watoto nao hawpo nyuma katika kuokota vitu vilivyo tupwa katika maguba hayo,Lakini pamoja na ukosefu wa vitendea kazi Basi angalau hata kwa kukodi malori yaende Kata ya Majego kuzoa taka hizo
Hiyo ni barabara ya Malori ambapo takataka zimo kando kando kwa barabara hiyo.
Barabara hiyi hujulikana kwa barabara ya nitmba,kama unavoona guba la takataka lipo jirani na wauza mitumba .
Hiyo ni bara bara ya majengo maarufu kwa barabara ya mitumba Naeng,ya Majengo



WANANCHI wa Kata ya Majengo Manispaa ya Songea wanailalamikia Halmashauri hiyo kuacha kupeleka gari la kuzoa taka hizo.Na kwamba wanadai kwa kuwa Diwani wao ni wa Chama cha Upinzani ndiyo maana Halmashsuri haipeleki gari huko
.
Kwa mujibu wa baadhi ya wananchi wa Kata hiyo ,walisema kuna maguba mengi tu ambayo hayajazolewa taka kwa muda mrefu na kusababisha harufu mbaya katika maeneo hayo ambayo yamezungukwa na makazi ya watu.

 Walisema inashangaza kuwaona viongozi wanapita na magari yao na kuziona taka hizo bila ya kuchukua hatua yoyote,kiafya haipendezi kuona watoto wanaokota vitu kwenye maguba hayo.Istoshe mbele ya guba moja kuna duka la madawa lililoandikwa HATI PUNGUZO.

Wananchi hao wasiwasi wao ni kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafu uliyo kithili,wanadai kuwa wanaona taka zilizo katikati ya mji na sokoni ndiyo zinazo zolewa.na kwao zinaendelea kusambaa.

Ambapo alipo ulizwa Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bwana Nachoa Zakaria alikiri kusema kuwa tatizo hilo linaeleweka na wala halina mahusiano na tofauti za vyama katika Manispaa yake.Bali manispaa haina magari ya kutosha.

Alisema tatizo lililopo ni la ukosefu wa vitendea kazi ambapo kwa sasa Manispaa ina malori mawili tu ambayo ni mabovu ni ya miaka 20 tangu yanunuliwe,kila siku ni gereji,na kwamba ili kusomba taka zote kunahitajika magari sita mapya ya tani 20 na kijiko.kwa ajili ya kuzolea taka,wakati sasa wanatumika vibarua kuzoe taka hizo kwa machepe.

No comments:

Post a Comment