Wednesday, May 8, 2013

BREAKING NEWS , KUUA MAASKOFU,MAPADRE AU MUFTI NA MASHEKHE NDIYO KUUMALIZA UKRISTO AU UISLAMU,NI KUJIDANGANYA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Pinda,alisema watu wasijidanganye hata kidogo,kwa kuzani kuwa wakiwaua viongozi wa dini ndiyo mwisho wa Ukristo au Uislamu.Hapana watu wataendelea na Imani zao.
Alisema kuwaua Maaskofu,Mapadre au Mufti na Mashekhe ndiyo mwisho wa Ukristo au Uislamu ni kujidaganya.kwani pale unaua Askofu ,Padre, Mufti au Shekhe basi siyo kuua Ukristo au Uislamu.

Kauli  hiyoaliitoa alipokuwa akizungumza  na wananchi wa Mkoa wa Arushu alipo kwenda kutoa pole kwa wahanga wa Bomu lililolipuliwa ndani ya Kanisa katoliki la Mt.Joseph Mfanyakazi.Na kuwataka wanachi watulie nakuwaombea majeruhi wapate nafuu mapema ili waungane na Jamaa zao.

Wakati huo huo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam Muadhama Policarp Pengo alisema Tukio lililotokea Arusha lisihusishwe na Uislamu kwa kuwa ndani ya wahalifu wanaodhaniwa kufanya uhalifu huo wamo pia na wakristo

No comments:

Post a Comment