Sunday, May 5, 2013

BEAKING NEWSS ,ARUSHA,MWAKILISHI WA PAPA FRANCI NCHINI TANZANIA ANUSURIKA KULIPULIWA NA BOMU MITA 10 TOKA LILIPOLIPUKA BOMU HILO LEO

Mwakilishi wa Papa Franci Nhini Tanzania amenusurika kulipuliwa na bomu lililolipuka umbali wa mita 10kutoka pale alipo, ndani ya Kanisa Katoliki la Olasite Jijini Arusha leo wakati akiendesha Ibada ya uzinduzi wa kanisa hilo.

Kwa mujibu wa Sechelela Kongola  TBC Arusha inasema watu wapatao 20 wameathirika na mlipuko huo,na majeruhi wamekimbizwa hospitalini kwa matibabu.

Aidha inasema ibada hiyo imesitishwa na waumini wameruhusiwa kurudi majumbani kwao,Mgeni ambaye ni mwakilishi wa Papa ,Askofu,Mapadre na Masista wamo ndaini ya majengo ya kanisa hilo kwa usalama na kusubili hali iwe shuwari.

Pamoja na tukio hilo hadi sasa haijajulikana kuwa bomu hilo liliwekwa na nani,na kama mtu aliweka  alikuwa na nia gani ya kutaka kupoteza maisha ya melufu ya waumini wa kanisa hilo wasio na hatia.

Serikali mkoani Arusha tayari imesha wasili katika kanisa hilo akiwemo ,Kamanda wa Polisi  wa mkoa wa Arusha  na kwamba uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha mlipuko huo na nani aliyehusika na tukio hilo.

Huwa tunasikia tu kuwa makanisa yanachomwa moto Zazibar leo,wa- Tanzania wameshuhudia Live mlipuko wa bomu, Hivi nchi hii imeingiliwa na Ugonjwa gani kwenye vichwa vya Watanzania ? tatizo liko  wapi, kama ni tikadi za vyama mbona kila mtu ni mfuasi wa chama fulani, haiwezekani kulazimishana kuingia kwenye chama ambacho mtu hakipendi.

Na hivyo hivyokwenye Imani za kidini kila mtu anaamua kufuata Dhehebu analoona akienda huko,huwenda akafika Mbinguni au kwa Mungu, Hatuwezi wote tukaenda kwenye madhehebu ambayo hatuyapendi. E Mungu, hebu angalia viumbe wako waliko, wamefikia hatua mbaya uwashushie upendo kupitia kwa Mitume wako uliyewatuma Duniani kuja kuwakomboa kutoka kwenye Utumwa wa dhambi. Wote tuna kuomba wewe, tofauti yetu ni majina tunayo kuita sisi wanadamu kulingana na makabila uliyo yagawa wewe mwenyewe Baba.

Lakini kama ni kikundi cha wafuasi au Itikkadi fulani, hawana nia nzuri kwa Taifa letu,Wameamua kuchafua jina la nchi yetu,watu wake na viongozi wake,huwenda kwa manufaa ya watu wachache wasiyopenda Amani ,Utulivu,Mshikamano na Umoja tulionao  Wa- tanzania

No comments:

Post a Comment