Saturday, May 18, 2013

MIUNDOMBINU YA RELI YA KATI IKIIMARISHWA PAMOJA NA KUIMARISHA NYUMBA ZA WAFANYA KAZI WA RELI HIYO IKIWA NA KUONGEZA WAFANYA NAZI NA MISHAHARA YA KUTOSHA HALI YA USAFIRISHAJI WA MIZIGO NA ABIRIA UTAKUWA KAMA AWALI

 Railway Station Kimamba kwa sasa pamefungwa kwa muda kushoto kwako ni jengo ambalo wasafiri wanakatia tiketi na ni ofisi ya Station Master.Unaingalia kuelekea Dar es Salaam
 Hiki ni kituo kidogo cha Train cha Kimamba Kilosa ( Station ) hiyo ni Reli mbayo bado ipo imara ingawa kituo hicho hakifanyiwi usafi kwa kuwa kimefungwa kwa muda.unaitazama ikielekea Dodoma.
 Hiyo nyumba ni ya Station Master
Hilo jengo la Station ya Mkata,Kwa mujibu wa Mfanya kazi katika Shirika la Reli katika Station ya Kilosa ambaye hakupenda jina lake lijulikane, aliiambia Blog hii leo kuwa.Vituo vyote vya Train havijafungwa na hali ya Njia ya Reli ni nzuri ila inatakiwa kubadilishwa.
Alisema kuanzia eneo la Kilosa hadi Mwenyimsagali reli yake bado ni ya Pound 65 ambayo Train kipita juu inachezacheza kwa kuwa ni nyembamba na kusababisha kuacha reli na kuanguka,ni tofauti na maeneo ambayo wametandika reli ya Pound 80.
Amesema hata hiyo ya Pound 80 imeshapitwa na wakati,pamoja na kwamba Reli ya Tazara ina uzito wa Pound 80.
Aidha amesema ili kufanikisha Reli hiyo Serikali ikarabati miundombinu yake,magenge ambayo kuna wafanya kazi wanaishi  huko na yenyewe yakarabatiwe,na wafanya kazi waongezwe mishahara kwani iliyopo ni midogo kulinga na kazi wanazozifanya za kunyanyua mataruma
Alisema kwenye Yard ambapo ni Railway Station panatakiwa kuwepo na wafanya kazi 9 na fundi mmoja kwa ajili ya kushusha na kutandika reli.

No comments:

Post a Comment