Friday, July 1, 2011

WANAFUNZI 7 WAFANYA VIZURI KATIKA MASOMO YA SAYANSI KIDATO CHA SITA 2011 KUTOKA SEKONDARI ZA KATA

 Serikali imewapongeza wanafunzi 20 waliyofanya vizuri katika masomo ya sayansi katika matokeo ya mitihani ya taifa ya kidato cha sita mwaka huu leo Bungeni,ambapo Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhe. Prf.Shukuru Kawambwa alipowafagilia walimu,wanafunzi na wazazi ambao kwa ushirikiano na walimu katika sekondari hizo zilizotoa wanafunzi hao zikiwemo na sekondari za kata kuwa waendelee na mshikamano huo.

Hao ni wanafunzi 20 wakiume 10 na wakike 10 ambapo kati ya wanafunzi hao waliyofanya maajabu katika masomo ya sayansi kidato cha sita mwaka 2011,kati yao wanafunzi 7 wametoka katika sekondari hizo za kata nchini wakiwa wameshika vyeti vyao walitunukiwa na Mhe.Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda Bungeni Dodoma masaa machache yaliyopita hivi leo.

No comments:

Post a Comment