Friday, July 15, 2011

UMEME UMESABABISHA WAKAZI WA SONGEA NA VITONGOJI VYAKE KUKOSA HUDUMA ZA KIBENKI LEO

 Umeme imekuwa gumzo leo mjini hapa,wengine wanasema huwenda mashine za kuzalisha umeme zimekufa,lakini wengine wanasema labda mafuta huwenda hakuna ,lakini mmoja ndiyo alitoa mpya kuwa mwenye kuleta mafuta katika mitambo ya kuzalisha umeme hulo kiblang'oma Manispaa ya Songea hajalipwa pesa yake.
Yote tisa lakini watu wapo mlangoni wakisubiri miujiza umeme uwake huduma za benki ziendelee,maana kila mmoja alikuwa na shida yake ya kutatua baada ya kupata pesa au kuweka pesa mahala pa usalama ambapo bila umeme kuzipata pesa hizo ni shughuli.
 Nishati hizi za umeme hapa mkoani Ruvuma ilikuwa ni kitu kidogo sana,kwani vyanzo vya upatikanaji wake ni rahisi mmno iwapo serikali ingevutia wawekezaji katika nishati ya umeme.Kuna maporomoko ya nakatuta yenye uwezo wa kuzlisha umeme,kuna makaa ya mawe yenye uwezo wa kuzalisha umeme isitoshe tuna Urenium namtumbo yote hayo yangeweza kuzalisha umeme wa uhakika,hata wenye Grid ya Taifa wasingfua dafu,Lakini yangoswe ni mwachie ngoswe mwenyewe,yetu ni kushuhudia jinsi nishati ya umeme isipopewa kipaumbele,Humo ni ndani ya Benki,unayoyaona ni Computer hizo,haziwezi kufanya kazi bila ya umeme je mfanyakazi akae mbele ya computer iliyo giza atamhudumia mteja?
 Hivyo hivyo kwenye ATM ni mtandao wa computer pia bila umeme huwezi kutoa pesa humo kwenye kisanduku hicho wao wajanja wanakiita ATM basi mradi wenye kushika tama,baki wenye kushika vichwa nao hivyohivyo pesa hakuna,kuna wenye wagonjwa hospitali wameambiwa wakanunue dawa,wengine wameambiwa wawe na shilingi 2,000/= za kumwona mgangaili amwandikie dawa akanunue maduka ya mitaani.Umeme huu jamani utaumbua watu kweli.Shida haina ujanja,lakini tutafika,wakati wenzetu wanapeta na umeme wa Grid ya Taifa Ruvuma tunavuma kwa kilimo,umeme wa mafuta anayoletwa kwa malori,Hivyo ni lini na wana - Ruvuma nao watakuwa na umeme wa uhakika?
 Nisiseme mengi mengine yanajieleza ukiziona picha hizo,ni jinsi gani wapiga kura hawa wanavyo kosa huduma muhimu.
Ni kawaida lakini kawaida haizoeleki hata chembe,wengine wanapeta kwa umeme wa Grid na wengine wanambulia Diesel ili mtambo uzalishe umeme unategemea nini,nakama Jenereta lenyewe ni la enzi ya Nuhu ni kila kukicha ICU.

No comments:

Post a Comment