Tuesday, July 19, 2011

KANDA ZA KUSINI NA ZIWA ZIMECHAPA MAGAZETI YA KISOMO ZAIDI YA 1000 NA KUYASAMBAZA

 Katika jitihada za kuwafikishia wananchi wa kisomo katika madarasa yao ya kisomo ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi,Kanda ya Kusini yenye mikoa ya Mtwara,Lindi na Ruvuma ambapo kituo cha Uchaoaji cha Kanda kilipo kilianza kuchapisha magazeti ya TUJIFUNZE  kama yanavyo onekana matoleo Na1 Agosti 2009 na toleo Na 2 Desemba 2009.
 Likafuatia Toleo Na.3 Januari 2010
Hatimaye Toleo Na 4 Mei 2010,na matoleo mengine katika Baadhi ya halmashauri zilitaka kuchapisha machapisho yao ya mafunzo juu ya ahtari ya virusi vya UKIMWI na ugonjwa wa UKIMWI halmashauri za Wilaya ya Songea Manispaa na Mbinga.
Katika maelezo ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa amesema Wizara yake imeweka malengo ya Uchapishaji wa magazeti hayo katika Kanda zake zote saba.Kutokana na Gazeti hilo ndipo Blog ya TUJIFUNZE KUSINI ikazaliwa kwa lengo la kutoa habari za kusini mwa - Tanzania na maeneo mengine nchini na nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment