Friday, July 1, 2011

Waliyofanya vizuri katika masomo ya sayansi kidato cha sita watunukiwa vyeti na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Bungeni Dodoma leo

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda amkabidhi cheti mwanafunzi Francis John aliyefanya vizuri katika masomo ya Sayansi Bungeni Dodoma leo.
Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe.Freeman Mbowe akimpongeza mwanafunzi Agapi Chacha aliyefanya maajabu katika masomo ya sayansi mtihani wa Taifa mwaka 2011 ndani ya Bunge leo mjini Dodoma masaa machache yaliyo pita.
 Mhe.Waziri mkuu akiwapongeza wanafunzi 20 kati yao wanafunzi 7 wanatoka katika sekondari za kata nchini
Mhe.Prf.Shukuru Kawambwa akitoa taarifa kwa Waheshimiwa wabunge kuwa wanafunzi na walimu wanafundisha katika shule ambazo wanafunzi hutokea kufanya vizuri zaidi ya wengine katika masomo ya sayansi ambayo wengi wao huyaona na magumu lazima watapongezwa na kupewa zawadi.



WAZIRI mkuu  Mizengo Pinda amewazawadia wanafunzi 20 Bungeni Mjini Dodoma leo baada ya kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa ya kidato cha nne mwaka 2011.

Wanafunzi hao 10 ni wavulana na 10 ni wasichana  waliyopewa vyeti baada ya kufanya maajabu katika masomo ya sayansi,zaidi ya hapo kati ya wanafunzi hao 20 kati yao wanafunzi 7 wametoka katika sekondari za kata ambazo wengi wanazidharau na kusema hazina maana.

Alisema serilikali inaona mbali katika kuanzisha Programu za kuboresha elimu nchini kama ilivyo katika MMEM na baadaye MMES ambayo ndiyo matunda ya shule za sekondari za kata nchini na matokeo yake yanaanza kuonekana kutokea wanafunzi waliyofanya vizuri zaidi katika masomo ya sayansi kama wale wa shule za serikali kongwe.

Aidha Mhe.Pinda amewaasa wanafunzi hao kuwa waepukane na migomo isiyo na tija wakati wa kuendelea na masomo ya elimu ya juu,alisema kuwa wasifuate makundi ambayo kwa namna moja au nyingine wanawaingiza hata wanafunzi ambao hawapo katika matarajio ya kufanya maadamano.

Amezitaja sekondari zilizotoa wanafunzi hao waliofanya vizuri wa kidato cha 6  kuwa ni pamoja na :-Kibaha,Mzumbe,D’salaam,Tabora Boys,Tabora Girls,Benjamini William Mkapa,Tanga,Kiloka,Arusha,Kilimanjaro , Mbeya na Kilakala Morogoro.



No comments:

Post a Comment