Saturday, July 2, 2011

LORI LA JERUHI 3 WAPELKWA HOSPITALI YA MKOA SONGEA BAADA YA KUTUMBUKIA DARAJANI MATARAWE LEO

 Watu watatu  ( 3 ) wamekimbizwa hospitali ya mkoa wa Songea leo asubuhi  baada ya lori walilo kuwa wakipeleka maturubai  SAMCO kutoka Ruhuwiko kwenye ghala la kuhifadhia chakula mkoa wa Ruvuma baada ya lori hilo kutumbukia kwenye daraja la Matarawe Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Watu kadhaa waliyo shuhudia ajali hiyo wamasema kuwa lori hilo lilikuwa limejaza maturubai,likiwa na matindo 32,hivyo lilivyovuka daraja na kupandisha mlima, lori hilo lilimshinda dereva na kurudi kisha kutumbukia darajani,kuona hivyo wote waliruka.ndipo watatu kati yao waliruka vibaya na kupata majeraha wote walikimbizwa hosipitali.
 Baadhi ya matingo waliyosalimika katika ajali hiyo wakiyavuta maturubai yaliyo mwagikia darajani,na mengine kutupwa ng'ambo ya daraja hilo dogo la Manispaa ya Songea lililoko Matarawe,ili kupakia kwenye lori lingine lililopelekwa katika tukio hilo.

1 comment: