Thursday, July 14, 2011

POSHO YA MIITO YA USIKU YA SHILINGI 10,000 KWA MADAKTARI NCHI HAITOSHI NDIYO INAWAFANYA KUFANYA KAZI ZA ZIADA

Viongozi wa Chama cha Madktari Nchini wasema tangu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamiikuingia madarakani hajawahi kukutana na Viongozi wa Chama cha Madaktari nchini kuzungumzia matatizo lukuki yanayo ikabili Sekta ya afya nchini. Hivyo ni juu ya waziri huyo kukutana na viongozi hao wanaweza kuwa na jambo la kuleta tija katika sekta ya afya japo wa nusu saa hivi atapata kitu cha muhimu kutoka kwa Madaktari viongozi hao.
Viongozi hao wanasema wanaipenda sana kazi yao kwa kuwa wamesomeshwa na Serikali yao,ila maslahi hayaendi na elimu waliyokuwa nayo,mazingira ya kufanyia kazi hayafanani ha elimu waliyo nayo.wametoa mfano wa posho inayotolewa ya miito ya usiku kwa Daktari bingwa ya shilingi 10,000/= kwa wakati wa leo haimsaidii daktari huyo.Maana hana usafiri labda adandie daladala toka Mbagala hadi Mhimbili,au akodi gara kwenda na kurudi hiyo 10,000/= bado ipo?

Lazima serikali kupitia Wizara ya Afya iwe na jicho la kuliona hilo,Zahanati nyingi zimejengwa kwa nguvu ya wananchi lakini hazina waganga,madawa,nyumba za waganga wenyewe au wahudumu.Bado kunachangamoto nyingi Wizara ya afya.

No comments:

Post a Comment