Thursday, July 14, 2011

ROSTAM ALIZA WAPIGA KURA WAKE WA JIMBO LA IGUNGA JANA

 Wananchi wa jimbo la Igunga jana hawakuamini kasikio yao waliposikia Mhe.Rostam Aziz akisema kuwa pamoja na kafanikio yote yaliyo patikana katika miaka yake ya Ubunge Jimboni humo, yakiwemo ya Elimu ,Afya na maji,sasa inatosha kwa kutoka moyoni mwake alisema anajiuzuru,Ujumbe wa NEC CCM na Ubunge.Ukweli wengi walilia toka moyoni mwao kutokana na yale Mhe. Aziz aliyoyafanya ya kupeleka maendeleo katika Jimbo hilo.Maana imekuwa kwa wa - Tanzania wengi kuwa wanafiki wa kujifanya wanalia kumbe wanasema afadhali achie ngazi ili hali ya Igunga iwe kama alivyoikuta,kwa kuwa uwezo wa kuifanya Igunga ya maendeleo hawatakuwa nao.Aziz hategemei fedha za Ubunge kuendeleza Igunga bali ni pamoja na fedha ndani ya familia yake ndizo zilizofanya Igunga ya leo.
 Lakini naye Kaimu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. John Joel anasema kuwa huo ni uvumi kwani Bunge halijapata habari za Mhe. Aziz kujiuzuru kwake.
Je kuhusu tukio hili la Mwana CCM kujivua katika madaraka yake,Bw.John Chiligati atasema nini ?

Kwa kawaida mtu napowafanyia watu maendeleo kwa faida yao siyo yake ni vyema kumshukuru wangapi matajiri nchi hii,wamefanya maendeleo katika maeneo yao licha yakuwa wao si wabunge wala wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM.Kwa kauli yake Mhe. Aziz Jana alisema "napisha marumbano ndani ya Chama changu na Vyama vingine yasiyo niletea faida katika maisha yangu" hiyo tu inatosha kuona ni jinsi gani binadamu alivyo na macho ya kuona kwa muda mfupi mambo mazuri na baadaya macho hayo hayo hayaoni tena jitihada za mtu yule yule aliyefanya mapindizi katika maendeleo  ya mahali husika au ya watu kadhaa nchini.Je hiyo ndiyo fadhila ya watu wanaojitoa mhanga katika kuwaletea maendeleo wananchi? au ndiyo tusema wamevaa miwani ya mbao yasiyoweza kupisha ukweli wa mambo?.

Sijui,tunashabikia lakini ukweli unabakia palepale mwenye uwezo ndiye atakaye saidia kuleta maendeleo,na asiye na uwezo atabakia kusema na kuwasema wenye uwezo,ndicho alicho nacho.Hii nakataa katu pesa ya ubunge wako bila ya miradi yako uliyokuwa nayo kabla ya kuingia jengoni ,halafu upeleke maendeleo katika jimbo lako mbona hiyo ni ndoto,Akina Aziz hao wako wengi wakiamua kufuata maelekezo yaliyotolewa ya kuachia ngazi waliyokuwamo jengoni matokeo yake mtayaona.Ingawa ni mabingwa wa kushabikia mambo.

No comments:

Post a Comment