Saturday, July 9, 2011

FAMILIA YA MAREHEMU CHIHOMO SOKONI LEO IMEWASHUKURU MAPADRE,MADAKTARI NARAFIKI WA MAREHEMU CHIHOMO SOKONI KWA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KUMBUKUMBU LEO MJINI SONGEA

Familia ya  Mama Sofia Kayanji Sokoni wa Manispaa ya Songea leo imefanya Ibada ya kumbumbu ya Mtoto wao Mpendwa Chihomo Sokoni aliyefariki Ijumaa kuu mwaka huu tarehe 22/4/2011 na kuzikwa siku ya mkesha wa sikukuu ya Pasaka tarehe 23/4/2011,familia hiyo imewashukuru Mapadre,waganga,majirani,marafiki wa karibu na Marehemu,na wote wenye mapenzi mema waliyoshiriki wakati wa kuugua,mazishi na hatimaye leo 40 na ibada yake ya shukrani kwa Mungu.Roho ya Marehemu Chihomo Sokoni ikae mahali pema peponi Amina.
 Mama Sofia Kayanja Sokoni akiwa pamoja na wote waliofika katika ibada hiyo iliyoongozwa na Padre John Mapunda wa Kanisa la Anglican Songea Mjini Leo.
 Mpendwa Mke wa marehemu Chihomo Sokoni Bibi Tarsisia Milinga akiwa bado na majonzi ya kuondokewa na Mumewe Mpendwa,lakini sisi kama binadamu kazi ya Mungu haina makosa ,Marehemu Chihomo Sokoni Mungu alimpenda zaidi,akamchukua,basi njia hiyo ni kwa kila mmoja wetu ataipitia.Pole sana kwa yote yaliyotokea.
 Watoto , wa marehemu,mama na ndugu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ibada ya kumbukumbu ya Marehemu Baba yao mpendwa Sokoni.
 Mjomba wa marehemu Chihomo Sokoni Daktari mstaafu Philipo Kayanja
 Mdogo wa Marehemu Bwana Amani Sokoni
 Mdogo wa Marehemu Chihomo Sokoni Bwana Yohani Sokoni
 Shemeji wa marehemu Chihomo sokoni Bwana Milinga wa Peramiho.
picha ya pamoja ya watoto wa marehemu na mama yao.yaha hapo chini.

No comments:

Post a Comment