Friday, July 8, 2011

kuharibika kwa Teller za kuchukulia fedha nje ya benki ya NMB tawi la Songea kwa sababisha msongamano benki

Kuharibika kwa visanduku vya kutolea fedha Tellers  katika tawi la NMB mjini Songea kumesababisha msongamano wa wateja  kujazana ndani ya benki hiyo leo kuchukua na kuweka fedha.
Blog hii leo imeshuhudia jinsi watu wanavyo laumu huduma mbovu katika benki hiyo.Wanajiuliza kama ma-teller hayo yameharibika kwanini wasingetengeneza na huduma ikaendelea kama juzi,Hivyo hawaoni karaha kuona umati wa watu ulivyo jazana ndani ya benki kwa muda mrefu.
Pamoja na NMB inawateja wengi lakini pia waliyopewa dhamana ya kuhudumia watu hawako makoni katika utendaji wao wa kazi.
Lakini kingine kinachochangia kwa hapa Songea ni kuwa na teller katika jengo la benki hiyo tu,badala ya kuweka katika vituo vya mafuta kama walivyofanya NBC tawi la Songea.

No comments:

Post a Comment