Bwana Rashid Holela akielezea jinsi malipo ya wastaafu yanavyocheleweshwa katika Benki ya NMB tawi la Songea.Alisema fedha walizo fika kuzichukua zilikuwa zilipwe mwezi wa tatu lakini hadi leo tarehe 29/4/2013 fedha hizo hazijaingizwa.
Wasomaji wa Blog hii picha hiyo ya Bw.Rashid siyo 'Action' hapana anasema kwa jaziba akionyesha wazee wezake waliyo kaa katika ukuta wa Benki ya NMB bila kujua hatima yao kuhusu pesa hizo.Akimwambia Ripota na Mwakilishi wa Radio UHURU Mkoa wa Ruvuma Bwana Juma Nyumayo, kuwa waambie na wazee wengine wanakoisikia Radio hiyo kuwa wawaunge mkono maana kilio hicho wanaamini ni cha wengi ' aliyeshiba hamjui mwenye njaa' alisema Bw.Rashid.
Bwana Rashid anasisitiza kuwa Serikali haiwatendei haki wazee waliofanya kazi serikalini wakiwa watumishi wa Umma. kwanza fedha tunazolipwa hazikidhi haja kutokana na maisha yalivyo kuwa magumu,pili pamoja na hicho kidogo kulipwa mapema, nacho kinacheleweshwa. Hivyo wanavyo fanya hivi hawaji kustaafu siku moja ? aliuliza Bw.Rashid.( Picha na Juma Nyumayo)
Hapa Bw.Holela akimwita mzee mwenzake Bw. Mapunda afike apige picha pamoja ili kilio hicho kisiwe chake peke yake,wakati walikuwa pamoja wakiahangaika wapi wapate fedha,maana za Pesheni wenye zao wamegoma kuwapa.
Huyo aliyesimama mwenye koti ndiye Mzee Tobiasi Mapunda kutoka Lituhi kuja Tawi la NMB Songea kufuatia Pesheni yake na kuambulia patupu.
Pamoja na kuwa na mwenzake Mzee mapunda lakini Bwana Holela Rashidi bado alikuwa akiendelea kulaumu utaratibu uliyo wekwa na Serikali wa kuwalipa Pesheni wastaafu kila baada ya miezi mitatu na kisha kupitiliza hadi miezi mnne.

WASTAAFU wa utumishi wa Umma
katika Mkoa wa Ruvuma ,wanaulalamikia utaratibu wa malipo yao ya Pesheni yanavyolipwa ambayo hayaende kama serikali ilivyo tamka ya kulipwa
kila baada ya miezi mitatu mitatu.
Wakizungumza na Blog hii leo
katika Manspaa ya Songea katika Tawi la Benki ya NMB walipo fika kuchukua fedha
zao za mpesheni hawakuyaamini macho yao
baada ya kukuta salio lao halitoshi.
Bwana Holela Rashidi anasema “
mpaka leo hii ni mwezi wa nne sasa hawajatuingizi fedha zetu za Pesheni ambazo
zilitakiwa tuzichukue mwezi wa tatu, walituambia kuwa watakuwa wanatulipa kila
baada ya miezi mitatu mitatu, lakini cha ajabu tunakwenda kwenye ITM kuangalia
salio hakuna kilicho ingizwa.”
“Tumiitumikia nchi hii, leo
serikali inatufanyia vitendo hivi, mbona ni manyanyaso makubwa sana, wengine
wanatoka mbali wilaya ya Mbinga kuja kufuata mafao yao na wanapoyakosa inawalazimu kukaa kwa
jamaa zao, ambapo huleta kero kwa wenyeji wao” Alisema Bw.Rashidi.
Naye
Mzee Tobias Mapunda ametoka Wilaya ya Mbinga,” anasema nimetoka Litui Wilaya ya
Mbinga kuja kuchukua pesheni yangu ya miezi mitatu kama
serikali ilivyo tuhaidi,lakini nilivyo angalia salio sikukuta fedha
iliyoingizwa.na leo ni tarehe 29 mwezi wa nne, na fedhi hiyo ilibidi tulipwe
tarehe 30 mwezi wa tatu”.
Aidha
alisema kuwa tulienda hazina ndogo ya Mkoa wa Ruvuma ,na huko tuliambiwa fedha
imishapelekwa Benki ya NMB Tawi la
Songea, lakini tulivyo fika kwa meneja wa Benki tawi hilo tuliambiwa fedha hazija fika, sasa
tumlaumu nani ? kati ya Hazina na Benki? Huo ndiyo utaratibu wa serikali au ni
utaratibu wa Hazina na Benki kuwaingiza Wastaafu katika madeni wasiyoyapanga ?
aliuliza mzee Mapunda kwa uchungu mkubwa.
Hicho
ndicho kilio cha wazee wa Utumishi wa Umma waliostaafu na walilitumikia taifa
hili na kuliacha na watumishi wengine ambao na wao kuna siku watakuwa wastaafu
kama walivyo wazee hao Hivyo waliopewa
dhama hiyo ya kuwatendea haki wazee hao wawahudumie wazee hao, sio wa mkoa wa Ruvuma
peke yao, bali ugonjwa huu upo kwa nchi nzima, la kuwabeza wazee,lakini
wanasahau kuwa na wao ni wazee wa baadaye.