Wednesday, October 26, 2011

WIKI LA KISOMO KUFANYIKA MANISPAA YA SONGEA KATA YA MAJENGO KWA MAONYESHO MBALIMBALI

 Afisa Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Bwana Nathaniel Yonas akizungumza na TUJIFUNZE KUSINI jana kwenye ofisi zao,kuwa maadhimisho ya Juma la Elimu Kiwilaya litafanyika katika Kata ya Majengo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Majengo.Lengo la maadhimisho hayo ni kujumuika na mataifa mengine Ulimwenguni kuadhimisha na kutathimini maendeleo ya elimu ya watu wazima.
 Bibi Rose Mwombeki ni Afisa Elimu Vielelezo wa Manispaa ya Songea yuko katika Idara ya Elimu ya Watu Wazima Katika Manispaa hiyo.Kauli mbiu ya mwaka huu ni miaka 50 ya uhuru,elimu ya watu wazima ni ukombozi.



Pia Bwana Mpangala Honoratus naye ni Afisa Elimu Kilimo wa Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Songea.








WIKI  la kisomo Elimu ya Watu   Kiwilaya litafanyika katika Kata ya Majengo kwenye shule ya msingi ya Majengo kwa kukagua mabanda kadhaa ya maonyesho ya vikundi vya MUKEJA,VIKOBA vinavyoendeshwa na Elimu ya Watu Wazima kuifanya jamii iondokane na ujinga wa kutojua kusoma,kuandika na kuhesaba na kuwa wajasiliamali.

Afisa Elimu ya Watu Wazima katika Manispaa ya Songea Bwana Nathaniel Yonas alisema hayo kwenye ofisi za TUJIFUNZE KUSINI hivi karibuni alipotembelea ofisi hizo na kuelezea jinsi maadhimisho hayo yatakavyo fanyika.

Bw.Yonas alisema katika maadhimisho hayo kutakuwepo na maonyesho kutoka kwenye vikundi vya uzalishaji mali vya MUKEJA NA VICOBA,ambapo wanaonyesha na pia watauza vitu vitakavyo onyeshwa.

Alivitaja vitu hivyo kuwa ni pamoja na ufugaji,kuna maziwa,mayai ambapo wakulima ni pamoja na mboga,matunda pamoja na Sayansi- Kimu.kwa ujumla wake kutakuwa na vikundi saba kutoka MUKEJA na VICOBA nao wataonyesha shughuli zao na kuuza.

Aidha alisema kuwa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Kituo cha Songea nayo itakuwa na maonyesho ya Moduli mbalimbali za masomo ya O Level na A Level kwa wanafunzi wa Taasisi hiyo na wa sekondari nyingine kwa ajili ya kusoma mada ambazo huwenda wasingezipata kutokana na uhaba wa vitabu katika shule za sekondari.

Pia alisema kituo cha ufundi stadi cha shule ya msingi Mfaranyaki chenye fani za useremali,uashi na sayansikimu vitashiriki katika maonyesho hayo.

Kituo cha ufundi Stadi Shule ya Msingi Mfaranyaki kina walimu watatu wa fani hizo wakiwemo mwalimu Simoni Humbuka wa fani ya Uashi,Bibi Salvins Mpunga wa Sayansi-Kimu na Bwana Kachanga Ndeka wa Useremala na Italia Mbano wa Sayansi _kimu

Maazimisho hayo ya Songea yaenda sawia na maazimisho ya miaka 50 ya UHURU wa Tanganyika ya kutafakari na kuoanisha mazuri na mabaya yaliyojitokeza ndani ya miaka 50 hiyo ya Uhuru katika Awamu zote nne za uongozi wa Urais katika nchi hii.Elimu hiyo ilivyo anza kashamili baadaye kulegalega na hatimaye kuanza tena kwa mfumo wa ujasiliamali na kujifunza.

No comments:

Post a Comment