Saturday, October 8, 2011

UKOSEFU WA AJIRA NCHINI VIJANA WENGI WANAKOSA CHA KUFANYA

Ukosefu wa ajira kwa vijana ndiyo chanzo cha vitendo viovu kufanyika nchini,leo Blog hii imeshuhudia jinsi vijana walivyo kuwa wengi katika Manispaa ya Songea ambao walikusanyika eneo la Mtini ambako kampuni ya simu za mkononi za Voda ilipoweka jukwaa lake ili kuitangaza bia ya safari kwa wanyaji.
Wakati kampuni ys simu za mkononi  kitoa peromosheni ya bia ya safari katika Manispaa ya Songea maeneo ya Mtini,vijana wengi walionekana wakaijaa ushudia wanenguaji wa promosheni hiyo.Hii inatia mashaka kuwa vijana wote hao hawanakazi

1 comment:

  1. Hao vijana wasiangalie upande mmoja tu, kwamba wamekosa ajira. Wawe na upeo wa kuangalia upande wa pili, kwamba kukosa ajira maana yake wana muda mwingi sana mikononi mwao.

    Muda huo wanaweza kuutumia kwa kujiendeleza kielimu. Hapa Songea na katika miji mbali mbali kuna maktaba. Hata Mbinga kuna maktaba. Nimewahi kuchangia vitabu katika maktaba ile, vya masomo ya ki-Ingereza.

    Badala ya kukaa vijiweni, vijana wawe wanatumia muda wao kujielimisha. Waende maktaba kila siku, kwa mfano. Wataambulia mengi na kujipanga katika ushindani uliopo katika uwanja wa ajira. Kwa mfano, kwa kusomasoma vitabu vya ki-Ingereza na majarida, watajiongezea ufahamu wa lugha hii, ambayo ni kikwazo pale wanaposhindana kwa mfano na wa-Kenya au wa-Ganda kwenye ajira.

    Mwaka jana kulikuwa na tamasha la elimu na ajira Dar es Salaam, ambalo liliandaliwa na kampuni ya Tripod Media. Mimi nami nilifanya mpango wa kushiriki, kwani nina kijikampuni changu ambacho nimekisajili hapa Marekani lakini nataka kukiingiza Tanzania kiweze kuchangia ajira angalau mbili tatu.

    Nililipia shilingi zaidi kidogo ya 300,000 ambayo ndio gharama ya kushiriki maonyesho yale, nikapanga meza yangu. Nilitaka nikutane na hao vijana niwaeleze shughuli zangu, na kama mmoja au wawili wangeonekana wanapenda na ni makini, ningeweza kuwapa ajira.

    Cha ajabu ni kwamba vijana wenyewe hawakuhudhuria. Na kwa ujumla, waliohudhuria maonyesho hayo zaidi ni watoto wa shule. Hapo nilipata ushahidi kwamba pamoja na matatizo yote ya kweli yaliyopo, vijana wenyewe wanachangia kwa kutokuwa makini.

    Taarifa za hayo maonyesho ya Dar ni hii hapa.

    ReplyDelete