Saturday, October 15, 2011

ADHABU YA KUWAFUKUZA MADIWANI WAKE WATANO UNACHAMA WACCM WA UKOSEFU WA MAADILI WAFUTWA

 Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Bwana Emmanuel Mteming'ombe wakati wa mchakato wa kunadi wagombea wa Ubunge na Udiwani.
Mtahiki Meya wa Manispaa ya Songea Bwana Charles Mhagama wakati akijinadi wakati wa kuwania Udiwani katika Manispaa ya Songea  ambaye baadhi ya Madiwani wa CCM na Wapinzani waliwanya fujo wakati wakimchagua katika wadhifa huo aliokuwa nao sasa,ingawa bado baadhi hawautambui wadhifa wake.




KAMATI ya Siasa ya Halmashuri kuu ya Mkoa Mkoani Ruvuma  kupitia kikao chake kilichokaa hivi karibuni kimefuta adhabu ya kuwafukuza uanachama Madiwani watano wa Chama Hicho kutokana na kile kilichodaiwa ukosefu wa maadili wakati wa kumchagua Meya wa Manispaa hiyo.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Bwana Emmanuel Mteming’ombe baada ya kupitia maelezo yaliyotolewa na Kamati ya siasa ya Wilaya ya kuwafukuza Madiwani hao,maelezo ya uteuzi wa Madiwani waliyofukuzwa uanachama na Kamati ya Siasa ya Wilaya,Kamati ya Mkoa imetengua uamuzi huo wa kuwafukuza madiwani hao uanachama. Na kuendelea na uanachama na udiwani wao kama mwanzo.

Aidha Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Mkoa kimesikitishwa sana na vurugu na fujo zilizojitokeza katika Baraza la Madiwani wa kuchagua Meya wa Manispaa hiyo ,kufuatia vurugu hizo Chama Cha Mapinduzi Kimekemea na kulaani tabia hiyo ya kufanya vurugu katika vikao ambazo ni kinyume na kanuni za vikao na si tabia ya viongozi wanaotokana na CCM.

Bwana Mteming’ombe alisema kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa   kimeamua kutoa semina kwa Madiwani wote wanaotokana na chama hicho ili kuwaelimisha weledi juu ya kusimamia utekelezaji mzuri katika Halmashauri zao.

Pamoja na mambo mengine hali tete ya Baadhi ya Madiwani bila kujali Itikadi zao bado wanashikilia hali ya kutomtambua Meya wa Halmashauri hiyo Mstahiki Meya Charles Mhagama wa CCM Mbele ya Mkuu wa Moa huo alipokuwa akikagua shughuli za maendeleo katika Manispaa hiyo.

No comments:

Post a Comment