Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mhe.Charles Mhagama akielezea umuhimu wa Magazeti ya Kanda za elimu yalivyosaidia kufuta ujinga baada ya kupata UHURU,katika ofisi ya Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI jana alipotembelea kuona na kutoa ushauri wa jinsi ya kuyaendeleza magazeti hayo kwa wananchi vijijini ambako magazeti mengine hayawafikiii kiurahisi.
Mhariri Msaidizi Bwana Juma Nyumayo aliyesimama akimpa faili la nakala za magazeti ya NURU YETU ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini - Mbeya.
Mhariri Mkuu wa Magazeti ya TUJIFUNZE KUSINI Bwana Christian Sikapundwa kipongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mhe.Charles Mhagama kwa Dhamana kubwa aliyopewa na wananchi ya kuwatumikia na kuiletea maendeleo Manispaa hiyo,bila kujali malumbano yanayosaidia kurudisha nyuma maendeleo ya Mji wa Songea.
Mhariri Msaidizi wa Tujifunze Ofisini kwake akizungumza na Mtahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama hayupo pichani jana.
Bwana Juma Nyumayo akimsikiliza kwa makini Meya wa manispaa ya songea Charles Mhagama baada ya kusaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mhariri TUJIFUNZE KUSINI jana.
Meya Mhagama akimsikiliza Mhariri wa TUJIFUNZE Bw.Sikapundwa hayupo pichani hapo jana kwenye ofisi hiyo.

Magazeti ya Kanda
yametoa mchango mkubwa katika vijiji miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
MAGAZETI ya elimu yametoa mchango mkubwa katika maeneo ya
vijiji ambako magazeti mengine yalikuwa hayafikiki kwa urahisi,isitoshe wakati
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akitaka kuleta maendeleo baada ya uhuru
,alianzisha Elimu ya Watu Wazima kwa lengo la kuondoa ujinga kwa wananchi wa
nchi hii.
Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Charles Mhagama
alisema hayo kwenye ofisi za Gazeti la TUJIFUNZE KUSINI wakati akiyapitia baadhi ya
nakala za magazeti hayo ya kanda zote saba za elimu yaliyo kuwa yakichapwa na
kusambazwa vijijini kwa bei ya Tsh.5
miaka ya nyuma.
Mstahiki Meya Mhagama alisema magazeti hayo wakati
yalipokuwa yakichapishwa wananchi wa Kanda ya Kusini waliweza kupata habari za
wenzao wa mikoa mingine,wa Mtwara walielewa habari za Songea,wa Mbinga walisoma
habari za Ruangwa, ‘ Hivyo serikali itoa
msaada ili magazeti hayo yaweze kuchapishwa na kusambazwa vjijini kama mwanzo.
Magazeti hayo yaliachwa kuchapishwa mwaka 1995 bada ya
mashirika yaliyokuwa yakitoa misaada kuacha kutoa misaada hiyo tena katika
Kanda,Lakini Kanda ya Kusini imeendelea Kuyachapisha tangu mwaka 2006 hadi sasa
ambapo sasa tunaandaa Toleo maalumu la miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Ni kweli, Mwalimu Nyerere alihamasisha elimu ya watu wazima nchini kote. Hii ni pamoja na juhudi zake za kuhamasisha elimu kwa watu wote, akisisitiza kuwa elimu haina mwisho na ni haki ya kila mtu.
ReplyDeleteNina hakika kuwa kama angekuwa hai, Mwalimu angesifia sana juhudi zenu za kuendesha gazeti la "Tujifunze Kusini." Nawatakieni kila la heri na mafanikio makubwa zaidi na zaidi.