Wednesday, October 12, 2011

BREAKING NEWS !!! KAIMU MKURUGENZI WA IDARA YA HABARI AWATAKA WAANDHISHI KUACHA KUWA MAHAKIMU

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bwana Raphael Hokororo amesema kuwa waandishi wa habari wamekuwa wao ndiyo mahakama,polisi kwa kuwahuumu wanawaandika,alisema hayo jana kwenye kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC akiwa Butiama Mkoani Mara kwenye maandalizi ya miaka 50 ya UHURU.

Bw.Hokororo amesema katika miaka 50 ya UHURU wa Tanzania Bara sekta ya habari imepiga hatua kubwa,katika kuelimisha waandishi wa habari,ambapo hapo mwanzi kulikuwa na chuo kimoja tu cha Nyegezi Mwanza cha wa Misionari kilikuwa kikitoa mafunzo ya cheti na stashahada na baadaye chuo cha uandishi wa habari cha Dar es salaa ( Tanzania School of Journalism) TSJ wa ngazi ya cheti stashahada na shahda na sasa nichuo kikuu.

Ila amesema kuwa vyombo vingi vya habari vinawatumia waandishi wa habari ambao hawajapata elimu ya utosha ya undishi wa habari na ni wengi wanachojali magazeti yao yanauzwa,aidha alisema maadili ya uandishi wa habari haufuatwi na baadhi ya waandishi wa vyombo hivyo.

Alitoa maagizo kwenye mkutano wa maafisa habari uliyofanyika Jijini Mbeya hivi karibuni kuwa waandishi wanaotumwa na vyombo vyao kuandika habari wasipewe tena bahasha zinazotolewa na waendesha warsha,semina na makongamano kwa kuwa bahasha hizo zinawabana waandishi ku - balance  story zao kwa kuogopa kumuuzi aliyetoa bahasha.

Wizara ya habari vijana na michezo ipo Butiama kwa maandalizi ya miaka 50 ya UHURU  wa Tanzania Bara ambapo tarehe 15  mwezi huu mwenge wa UHURU utawashwa.


No comments:

Post a Comment