Thursday, October 27, 2011

NINANI ANAYE BEZA SEKONDARI WA KATA NCHINI ?

 Mkuu wa shule ya sekondari Kingerikiti Wilyani mbinga Mkoa wa Ruvuma Bwana Gisbert Kilian Kapinga Box 262 MBINGA Mob: 0788609366 akiwa ofisi za TUJIFUNZE KUSINI akifuatia Mock ya wilaya kwa Kidato cha Kwanza na Tatu inayochapwa TUJIFUNZE KUSINI
 Mkuu wa shule sekondari mikaranga Mbinga Bwana Francis Mwella ( Box 38 MBINGA Mob. 0756- 095848 ) maoni kuhusu mafanikio na changamoto zinazojitokeza kwenye sekondari za kata nchini.
Wakuu hao wakiwa ofisi ya TUJIFUNZE KUSINI wakijadili namna ya kuboresha zaidi Taaluma katika shule za sekondari za kata katika wilaya ya Mbinga,ambapo hatua ya kwanza wameanza kuchapisha mitihani ya wilaya yenye mfanano na mitihani ya mwisho ya kidato cha nne na sita.



SEKONDARI za kata nchini Tanzania zanamchango mkubwa kwa vijana ambao wangekosa nafasi ya kusoma elimu ya sekondari za serikali zilizoko na kuonyesha mafanikio makubwa kwa kutoa taaluma kama sekondari nyingine zilizoko iwapo kasoro ndogondogo zilizopo.

Usemi huu umetolewa leo na walimu wakuu wa shule za sekondari Wilaya ya Mbinga,ambapo Bwana Francis Mwella mkuu wa shule  Mikaranga Mbinga anasema kuwa kunawalimu 9 kutoka chuo kikuu Mlimani walifika kwenye mazoezi ya kufundisha, lakini kati ya hao 9 walimu watatu walisoma katika sekondari ya kata mikaranga.

Alisema kuwa kati ya mwaka 2006 hadi 2010 wanafunzi 42 wapo kidato cha tano na sita ambao wamesoma katika sekondari hiyo ya kata. ( 0788609366 ) kwa ufafanuzi zaidi wa mafanikio ya Sekondari za kata nchini.

Naye Mkuu wa shule wa Kingerikiti Bwana Gisbert Kilian Kapinga anasema kuna wanafunzi 40 waliyosoma shule ya sekondari ya kata Kingerikiti kati yao wanafunzi wane ( 4 ) wapo chuo kikuu mwaka wa kwanza.waliyo baki wapo A level ( Box 38, Mbinga,Mob. O756- 095848 ) iwapo utapenda kutoa maoni zaidi kuhusu sekondari za kata nchini Tanzania.

Aidha wakuu hao walisema kuwa iwapo changamoto ndogo ndogo zikitatuliwa shule hizo niza mafaniko makubwa. Walizitaja changamoto hizo kuwa ni mapoja na upungufu wa walimu hasa wa sayansi,maabara ya sayansi na vifaa vyake,miundombinu na kuwekea vipaumbele vya kutolea elimu katika shule hizo.

Shule za sekondari Wilaya ya Mbinga zenye umeme ni pamoja na Mikaranga sekondari wa jenereta la shule,Mkinga sekondari wa Sola,Lundo sekondari wa Sola na Kindimba sekondari umeme wa maji,njia ya kuelekea Litembo.

Wanaodharau sekondari za kata ,kama hazingekuwepo hao walienda vyuo vikuu kutoka wilaya moja tu wangekuwa wapi? Je Tanzania ina Skondari hizo ngapi? Kama idadi itakuwepo zimetoa wanafunzi wangapi waliyopo elimu ya juu?.




No comments:

Post a Comment