Tuesday, October 18, 2011

WATU 64,000 MOANI RUVUMA WAPO MAJUMBANI WENYE MAGONJWA YA AILI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Sasi ya RUVUMA MENTAL DISABILITIES ( RUMED ) Bwana Dadid Kakoyo akisoma Gazeti la TUJIFUNZE KUSINI kwenye ofisi ya Gazeti hilo kabla ajasaini kitabu cha wageni hapo jana alipotembelea kituo hicho.
Bwana Kakoyo anasaini kitabu cha wageni,TUJIFUNZE KUSINI inaanda Toleo Maalumu la miaka 50 ya UHURU,hivyo wageni wengi wanatembelea ili kujifunza ELIMU YA WATU WAZIMA MIAKA 50 ya UHURU imefanya nini katika Machapisho ya Magazeti ya Kisomo.
 Bw.Kikoyo akitoa maelezo namna ya kumsaidia mtu mwenye ugonjwa wa akili na kumweka katika mazingra ambayo yeye anajikuta yuko salama.kwa Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI Bwana Juma Nyumayo aliyeshika kudevu akimsikiliza kwa makini mtaalamu huyo.
Hapo anamwambia Mhariri huyo kuwa magonjwa ya akili yanatokana na watu kujihusisha na madawa ya kulevya,kukata tamaa na kujiingiza kwenye ulevi wa kupindiia,na kukataliwa na familia zao,kwa kukosa amani,upendo na matumaini hivyo wanasononeka ( SONONA ).

KUTOKANA na tawimu za Mkoa wa Ruvuma zinaonyesha wagonjwa akili 64,000 wapo majumbani hawajatamuliwa bado,inaonyesha katika nyumba moja katika wilaya ya Namtumbo kuna mtu moja ama wawili wana matatizo ya aili.

Akizungumza kwenye ofisi za TUJIFUNZE KUSINI jana Mkuruganzi mtendaji wa  RUVUMA MENTAL DISABILITIES ( RUMED ) Bwana David Kakoyo,kuwa tafiti kadhaa zimeonyesha Mkoa una watu wengi wanaougua magonjwa ya akili lakini bado wako majumbani.

Bw.Kakoyo alisema kuwa hadi sasa ni wagonjwa 792 ndiyo waliyotambuliwa kimkoa,Mbamba – Bay,Mbinga , Namtumbo,Songea Vijijini, ambapo tafiti zimefanyika na kuwapata wagonjwa  kuwanzishiwa matibabu.
     Aidha alisema ubongo wa binadamu unahitaji msaada mkubwa sana wa ushauri nasaha,alisema katika kituo chao kitu cha kwanza wakimpata mgonjwa wa akili wanampiga na maji, na kumpa ushauri nasaha ili ajue kuwa yupo salama.
     Alisema watu wenye nia mbaya na watu wengine wanaweza kuutumia ubongo wa mtu mwingine kwa lengo baya,na kumfanya mtu yule akawa kama mtumwa wake akamtumia vile anavyo taka.
     Kuhusu kituo chake alisema kuwa anategemea kupata watoto 30 mwaka ujao ambao wana matatizo ya akili,alisema pamoja na asasi yake kujishughulisha na magonjwa ya akili lakini pia ametoa ushauri na saha kwa mabinti wawili yatima.
      Kufuatia ushauri huo mabinti hao sasa wanasoma elimu ya juu,ambapo mmoja amehifadhiwa anasoma mwaka wa pili Chuo Kikuu Mtwara tawi la SAUT,na wapili anasoma chuo kikuu cha ushirika Moshi.
      RUVUMA MENTAL DISABILITIES ( RUMED) wanapata msaada kutoka wa The Foundation for Civil Society .
      Bwana Kakoyo alianza utafiti kwa watu wenye magonjwa ya akili mwaka 2001 Wilayani Mbinga,mwaka 2006 alifanya utambulisho wa asasi yake na mwaka 2007 hadi 2009 ikafika hadi Wilayani kuanzia hapo Asasi hii ipo katika viwanja vya Sabasaba Matarawe mkoani Ruvuma  ndiyo makao makuu yalipo.





No comments:

Post a Comment