Saturday, October 15, 2011

MKUU WA MKOA WA RUVUMA AFUNGUA KIKAO CHA WADAU WA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI SONGEA



 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said  Mwambungu akiwa Ofisini kwake akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa huo,leo amezungumza na wadau wa Habari na Waandishi wa habari katika ukumbi wa CWT katika Manispaa ya Songea.
 Katibu Mkuu wa Ruvuma Press Club  aliyesika karatasi akiwa na mdau wa Habari Bibi Mwenda wa wanza mwenye suti ya mistari kabla ya kikao kuanza.
 Baadhi ya waandishi wa Habari wakisubiri kikao kuanza na kutuma habari kwenye vyombo vyao wanavyo viandikia.
 Bibi Joyce Joliga  mwandishi wa habari mwenye suti ya zambarao  nyepesi wakibadilishana mawazo na Bibi mdau wa habari na mjumbe wa kamati  ya Maadili Katika Club ya Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa huo.


MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu afungua kikao cha siku moja cha wadau wa Habari na waandishi wa Habari leo katika ukumbi wa CWT katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.

Bw. Mwambungu amewataka wadau wa habari utoa habari kwa waandishi wa habari kwani bila ushirikiano wao na waandishi wa habari wananchi watakosa habari ambazo ni haki yao kuzielewa.

Aidha na waandishi wa habari nao wanawajibika kufuata maadili ya kazi yao ya kuandika habari bila kuegemea upande mmoja,ambazo haziwezi kuumiza mtu au kumnufaisha mtu kwa matakwa yake.

Kikao hicho kimejumuisha waandishi wa mkoa wote wa Ruvuma na wadau kadhaa kutoka katika Manispaa ya Songea.



No comments:

Post a Comment