Habari zilizopatikana kutokana baadhi ya watu waliyokuwepo kwenye Lori hilo inasema kuwa askari wawili majana yao hayakupatikana mara moja wameumia,na baadhi yao ni wazima.Habari zaidi utazipata kwenye vyombo vya habari.
Thursday, October 27, 2011
NINANI ANAYE BEZA SEKONDARI WA KATA NCHINI ?
Mkuu wa shule ya sekondari Kingerikiti Wilyani mbinga Mkoa wa Ruvuma Bwana Gisbert Kilian Kapinga Box 262 MBINGA Mob: 0788609366 akiwa ofisi za TUJIFUNZE KUSINI akifuatia Mock ya wilaya kwa Kidato cha Kwanza na Tatu inayochapwa TUJIFUNZE KUSINI
Mkuu wa shule sekondari mikaranga Mbinga Bwana Francis Mwella ( Box 38 MBINGA Mob. 0756- 095848 ) maoni kuhusu mafanikio na changamoto zinazojitokeza kwenye sekondari za kata nchini.
Wakuu hao wakiwa ofisi ya TUJIFUNZE KUSINI wakijadili namna ya kuboresha zaidi Taaluma katika shule za sekondari za kata katika wilaya ya Mbinga,ambapo hatua ya kwanza wameanza kuchapisha mitihani ya wilaya yenye mfanano na mitihani ya mwisho ya kidato cha nne na sita.
Mkuu wa shule sekondari mikaranga Mbinga Bwana Francis Mwella ( Box 38 MBINGA Mob. 0756- 095848 ) maoni kuhusu mafanikio na changamoto zinazojitokeza kwenye sekondari za kata nchini.
Wakuu hao wakiwa ofisi ya TUJIFUNZE KUSINI wakijadili namna ya kuboresha zaidi Taaluma katika shule za sekondari za kata katika wilaya ya Mbinga,ambapo hatua ya kwanza wameanza kuchapisha mitihani ya wilaya yenye mfanano na mitihani ya mwisho ya kidato cha nne na sita.
SEKONDARI za kata nchini Tanzania
zanamchango mkubwa kwa vijana ambao wangekosa nafasi ya kusoma elimu ya
sekondari za serikali zilizoko na kuonyesha mafanikio makubwa kwa kutoa taaluma
kama sekondari nyingine zilizoko iwapo kasoro
ndogondogo zilizopo.
Usemi huu umetolewa leo na walimu wakuu wa shule za
sekondari Wilaya ya Mbinga,ambapo Bwana Francis Mwella mkuu wa shule Mikaranga Mbinga anasema kuwa kunawalimu 9
kutoka chuo kikuu Mlimani walifika kwenye mazoezi ya kufundisha, lakini kati ya
hao 9 walimu watatu walisoma katika sekondari ya kata mikaranga.
Alisema kuwa kati ya mwaka 2006 hadi 2010 wanafunzi 42 wapo
kidato cha tano na sita ambao wamesoma katika sekondari hiyo ya kata. ( 0788609366 ) kwa ufafanuzi zaidi wa
mafanikio ya Sekondari za kata nchini.
Naye Mkuu wa shule wa Kingerikiti Bwana Gisbert Kilian
Kapinga anasema kuna wanafunzi 40 waliyosoma shule ya sekondari ya kata
Kingerikiti kati yao
wanafunzi wane ( 4 ) wapo chuo kikuu mwaka wa kwanza.waliyo baki wapo A
level ( Box 38,
Mbinga,Mob. O756- 095848 ) iwapo utapenda kutoa maoni zaidi kuhusu
sekondari za kata nchini Tanzania.
Aidha wakuu hao walisema kuwa iwapo changamoto ndogo ndogo
zikitatuliwa shule hizo niza mafaniko makubwa. Walizitaja changamoto hizo kuwa
ni mapoja na upungufu wa walimu hasa wa sayansi,maabara ya sayansi na vifaa
vyake,miundombinu na kuwekea vipaumbele vya kutolea elimu katika shule hizo.
Shule za sekondari Wilaya ya Mbinga zenye umeme ni pamoja na
Mikaranga sekondari wa jenereta la shule,Mkinga sekondari wa Sola,Lundo
sekondari wa Sola na Kindimba sekondari umeme wa maji,njia ya kuelekea Litembo.
Wanaodharau sekondari za kata ,kama
hazingekuwepo hao walienda vyuo vikuu kutoka wilaya moja tu wangekuwa wapi? Je Tanzania ina
Skondari hizo ngapi? Kama idadi itakuwepo
zimetoa wanafunzi wangapi waliyopo elimu ya juu?.
Wednesday, October 26, 2011
WIKI LA KISOMO KUFANYIKA MANISPAA YA SONGEA KATA YA MAJENGO KWA MAONYESHO MBALIMBALI
Afisa Elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma Bwana Nathaniel Yonas akizungumza na TUJIFUNZE KUSINI jana kwenye ofisi zao,kuwa maadhimisho ya Juma la Elimu Kiwilaya litafanyika katika Kata ya Majengo kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Majengo.Lengo la maadhimisho hayo ni kujumuika na mataifa mengine Ulimwenguni kuadhimisha na kutathimini maendeleo ya elimu ya watu wazima.
Bibi Rose Mwombeki ni Afisa Elimu Vielelezo wa Manispaa ya Songea yuko katika Idara ya Elimu ya Watu Wazima Katika Manispaa hiyo.Kauli mbiu ya mwaka huu ni miaka 50 ya uhuru,elimu ya watu wazima ni ukombozi.
Pia Bwana Mpangala Honoratus naye ni Afisa Elimu Kilimo wa Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Songea.
Bibi Rose Mwombeki ni Afisa Elimu Vielelezo wa Manispaa ya Songea yuko katika Idara ya Elimu ya Watu Wazima Katika Manispaa hiyo.Kauli mbiu ya mwaka huu ni miaka 50 ya uhuru,elimu ya watu wazima ni ukombozi.
Pia Bwana Mpangala Honoratus naye ni Afisa Elimu Kilimo wa Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Songea.
WIKI la kisomo Elimu ya Watu Kiwilaya litafanyika katika Kata ya Majengo
kwenye shule ya msingi ya Majengo kwa kukagua mabanda kadhaa ya maonyesho ya
vikundi vya MUKEJA,VIKOBA vinavyoendeshwa na Elimu ya Watu Wazima kuifanya
jamii iondokane na ujinga wa kutojua kusoma,kuandika na kuhesaba na kuwa
wajasiliamali.
Afisa Elimu ya Watu Wazima katika
Manispaa ya Songea Bwana Nathaniel Yonas alisema hayo kwenye ofisi za TUJIFUNZE
KUSINI hivi karibuni alipotembelea ofisi hizo na kuelezea jinsi maadhimisho
hayo yatakavyo fanyika.
Bw.Yonas alisema katika
maadhimisho hayo kutakuwepo na maonyesho kutoka kwenye vikundi vya uzalishaji mali vya MUKEJA
NA VICOBA,ambapo wanaonyesha na pia watauza vitu vitakavyo onyeshwa.
Alivitaja vitu hivyo kuwa ni
pamoja na ufugaji,kuna maziwa,mayai ambapo wakulima ni pamoja na mboga,matunda
pamoja na Sayansi- Kimu.kwa ujumla wake kutakuwa na vikundi saba kutoka MUKEJA
na VICOBA nao wataonyesha shughuli zao na kuuza.
Aidha alisema kuwa Taasisi ya
Elimu ya Watu Wazima Kituo cha Songea nayo itakuwa na maonyesho ya Moduli
mbalimbali za masomo ya O Level na A Level kwa wanafunzi wa Taasisi hiyo na wa
sekondari nyingine kwa ajili ya kusoma mada ambazo huwenda wasingezipata
kutokana na uhaba wa vitabu katika shule za sekondari.
Pia alisema kituo cha ufundi
stadi cha shule ya msingi Mfaranyaki chenye fani za useremali,uashi na
sayansikimu vitashiriki katika maonyesho hayo.
Kituo cha ufundi Stadi Shule ya Msingi
Mfaranyaki kina walimu watatu wa fani hizo wakiwemo mwalimu Simoni Humbuka wa
fani ya Uashi,Bibi Salvins Mpunga wa Sayansi-Kimu na Bwana Kachanga Ndeka wa
Useremala na Italia Mbano wa Sayansi _kimu
Maazimisho hayo ya Songea yaenda
sawia na maazimisho ya miaka 50 ya UHURU wa Tanganyika ya kutafakari na
kuoanisha mazuri na mabaya yaliyojitokeza ndani ya miaka 50 hiyo ya Uhuru
katika Awamu zote nne za uongozi wa Urais katika nchi hii.Elimu hiyo ilivyo
anza kashamili baadaye kulegalega na hatimaye kuanza tena kwa mfumo wa
ujasiliamali na kujifunza.
Thursday, October 20, 2011
WAGENI WENGI WANATEMBELEA MITAMBO YA UCHAPAJI TUJIFUNZE KUSINI KUJIFUNZA
Wgeni kutoka chuo cha ualimu Songea Mhasibu na Boharia walitembezwa kiwandani hapo jana.
wanaonyeshwa mashine ya kushona ( stitching machine )
wakionyeshwa mtambo mdogo wa uchapaji GTO
Wakionyeshwa mtambo mkubwa wa uchapishaji SORK
Wakionyeshwa meza ya kuandalia kazi ( Light Ta ball )
waimsikiliza fundi wa mashine kubwa ya uchapishaji akielezea akiwa juu.
wanaangalia mashine hizo kwa maini
wakiwa nje ya ofisi ya TUJIFUNZE KUSINI wakiaga.
MAGAZETI VIJIJINI YAMESAIDIA SANA KUFUTA UJINGA NCHINI KATIKA MIAKA 50 YA UHURU
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mhe.Charles Mhagama akielezea umuhimu wa Magazeti ya Kanda za elimu yalivyosaidia kufuta ujinga baada ya kupata UHURU,katika ofisi ya Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI jana alipotembelea kuona na kutoa ushauri wa jinsi ya kuyaendeleza magazeti hayo kwa wananchi vijijini ambako magazeti mengine hayawafikiii kiurahisi.
Mhariri Msaidizi Bwana Juma Nyumayo aliyesimama akimpa faili la nakala za magazeti ya NURU YETU ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini - Mbeya.
Mhariri Mkuu wa Magazeti ya TUJIFUNZE KUSINI Bwana Christian Sikapundwa kipongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mhe.Charles Mhagama kwa Dhamana kubwa aliyopewa na wananchi ya kuwatumikia na kuiletea maendeleo Manispaa hiyo,bila kujali malumbano yanayosaidia kurudisha nyuma maendeleo ya Mji wa Songea.
Mhariri Msaidizi wa Tujifunze Ofisini kwake akizungumza na Mtahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama hayupo pichani jana.
Bwana Juma Nyumayo akimsikiliza kwa makini Meya wa manispaa ya songea Charles Mhagama baada ya kusaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mhariri TUJIFUNZE KUSINI jana.
Meya Mhagama akimsikiliza Mhariri wa TUJIFUNZE Bw.Sikapundwa hayupo pichani hapo jana kwenye ofisi hiyo.
Mhariri Msaidizi Bwana Juma Nyumayo aliyesimama akimpa faili la nakala za magazeti ya NURU YETU ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini - Mbeya.
Mhariri Mkuu wa Magazeti ya TUJIFUNZE KUSINI Bwana Christian Sikapundwa kipongeza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mhe.Charles Mhagama kwa Dhamana kubwa aliyopewa na wananchi ya kuwatumikia na kuiletea maendeleo Manispaa hiyo,bila kujali malumbano yanayosaidia kurudisha nyuma maendeleo ya Mji wa Songea.
Mhariri Msaidizi wa Tujifunze Ofisini kwake akizungumza na Mtahiki Meya wa Manispaa ya Songea Charles Mhagama hayupo pichani jana.
Bwana Juma Nyumayo akimsikiliza kwa makini Meya wa manispaa ya songea Charles Mhagama baada ya kusaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Mhariri TUJIFUNZE KUSINI jana.
Meya Mhagama akimsikiliza Mhariri wa TUJIFUNZE Bw.Sikapundwa hayupo pichani hapo jana kwenye ofisi hiyo.
Magazeti ya Kanda
yametoa mchango mkubwa katika vijiji miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
MAGAZETI ya elimu yametoa mchango mkubwa katika maeneo ya
vijiji ambako magazeti mengine yalikuwa hayafikiki kwa urahisi,isitoshe wakati
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere akitaka kuleta maendeleo baada ya uhuru
,alianzisha Elimu ya Watu Wazima kwa lengo la kuondoa ujinga kwa wananchi wa
nchi hii.
Meya wa Manispaa ya Songea Mheshimiwa Charles Mhagama
alisema hayo kwenye ofisi za Gazeti la TUJIFUNZE KUSINI wakati akiyapitia baadhi ya
nakala za magazeti hayo ya kanda zote saba za elimu yaliyo kuwa yakichapwa na
kusambazwa vijijini kwa bei ya Tsh.5
miaka ya nyuma.
Mstahiki Meya Mhagama alisema magazeti hayo wakati
yalipokuwa yakichapishwa wananchi wa Kanda ya Kusini waliweza kupata habari za
wenzao wa mikoa mingine,wa Mtwara walielewa habari za Songea,wa Mbinga walisoma
habari za Ruangwa, ‘ Hivyo serikali itoa
msaada ili magazeti hayo yaweze kuchapishwa na kusambazwa vjijini kama mwanzo.
Magazeti hayo yaliachwa kuchapishwa mwaka 1995 bada ya
mashirika yaliyokuwa yakitoa misaada kuacha kutoa misaada hiyo tena katika
Kanda,Lakini Kanda ya Kusini imeendelea Kuyachapisha tangu mwaka 2006 hadi sasa
ambapo sasa tunaandaa Toleo maalumu la miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.
Tuesday, October 18, 2011
MIAKA 50 YA UHURU OFISI YA TUJIFUNZE KUSINI INAANDAA TOLEO MAALUMU ,MAONI YA NAKARIBISHWA KUHUSU ELIMI YA WATU WAZIMA TANZANIA
Maoni na mafaniio mbali mbali yanayo jitokeza ndani ya miaka 50 ya UHURU yanazidi kutolewa,nawe unaweza kutoa kupitia Blog hii ama E - mail.christiansikapundwa@yahoo.com.nasi tutachapisha kwenye Toleo Maalimu la mwezi Oktoba - Desemba ,karibu sana Motto wetu ( ELIMU HAINA MWISHO )
Ofisini kwa Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE Bw.Juma Nyumayo anapiga picha ambapo nakala za magazeti hayo zinapatikana.
Huo ni mtambo wa kuchapishia Magazeti ya TUJIFUNZE KUSINI ambapo sasa linaandaliwa Toleo maalumu la miaka 50 ya UHURU..Fundi Bw.W.Kaimbe anawaelekeza wageni unavyo fanya kazi.
Hizo mezani ni nakala za matoleo ya magazeti ya Kanda 8 za elimu hapo awali zilizojumuisha na Zanzibar ambapo Mhariri wake alikuwa Bwana Salim Salim mwandishi mwandamizi maarufu sana Zanzibar sasa.
Ofisini kwa Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE Bw.Juma Nyumayo anapiga picha ambapo nakala za magazeti hayo zinapatikana.
Huo ni mtambo wa kuchapishia Magazeti ya TUJIFUNZE KUSINI ambapo sasa linaandaliwa Toleo maalumu la miaka 50 ya UHURU..Fundi Bw.W.Kaimbe anawaelekeza wageni unavyo fanya kazi.
Hizo mezani ni nakala za matoleo ya magazeti ya Kanda 8 za elimu hapo awali zilizojumuisha na Zanzibar ambapo Mhariri wake alikuwa Bwana Salim Salim mwandishi mwandamizi maarufu sana Zanzibar sasa.
WATU 64,000 MOANI RUVUMA WAPO MAJUMBANI WENYE MAGONJWA YA AILI
Mkurugenzi Mtendaji wa Sasi ya RUVUMA MENTAL DISABILITIES ( RUMED ) Bwana Dadid Kakoyo akisoma Gazeti la TUJIFUNZE KUSINI kwenye ofisi ya Gazeti hilo kabla ajasaini kitabu cha wageni hapo jana alipotembelea kituo hicho.
Bwana Kakoyo anasaini kitabu cha wageni,TUJIFUNZE KUSINI inaanda Toleo Maalumu la miaka 50 ya UHURU,hivyo wageni wengi wanatembelea ili kujifunza ELIMU YA WATU WAZIMA MIAKA 50 ya UHURU imefanya nini katika Machapisho ya Magazeti ya Kisomo.
Bw.Kikoyo akitoa maelezo namna ya kumsaidia mtu mwenye ugonjwa wa akili na kumweka katika mazingra ambayo yeye anajikuta yuko salama.kwa Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI Bwana Juma Nyumayo aliyeshika kudevu akimsikiliza kwa makini mtaalamu huyo.
Hapo anamwambia Mhariri huyo kuwa magonjwa ya akili yanatokana na watu kujihusisha na madawa ya kulevya,kukata tamaa na kujiingiza kwenye ulevi wa kupindiia,na kukataliwa na familia zao,kwa kukosa amani,upendo na matumaini hivyo wanasononeka ( SONONA ).
Bwana Kakoyo anasaini kitabu cha wageni,TUJIFUNZE KUSINI inaanda Toleo Maalumu la miaka 50 ya UHURU,hivyo wageni wengi wanatembelea ili kujifunza ELIMU YA WATU WAZIMA MIAKA 50 ya UHURU imefanya nini katika Machapisho ya Magazeti ya Kisomo.
Bw.Kikoyo akitoa maelezo namna ya kumsaidia mtu mwenye ugonjwa wa akili na kumweka katika mazingra ambayo yeye anajikuta yuko salama.kwa Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE KUSINI Bwana Juma Nyumayo aliyeshika kudevu akimsikiliza kwa makini mtaalamu huyo.
Hapo anamwambia Mhariri huyo kuwa magonjwa ya akili yanatokana na watu kujihusisha na madawa ya kulevya,kukata tamaa na kujiingiza kwenye ulevi wa kupindiia,na kukataliwa na familia zao,kwa kukosa amani,upendo na matumaini hivyo wanasononeka ( SONONA ).
KUTOKANA na tawimu za Mkoa wa Ruvuma zinaonyesha wagonjwa akili 64,000 wapo majumbani hawajatamuliwa bado,inaonyesha katika nyumba
moja katika wilaya ya Namtumbo kuna mtu moja ama wawili wana matatizo ya aili.
Akizungumza kwenye ofisi za TUJIFUNZE KUSINI
jana Mkuruganzi mtendaji wa RUVUMA MENTAL DISABILITIES ( RUMED ) Bwana
David Kakoyo,kuwa tafiti kadhaa zimeonyesha Mkoa una watu wengi wanaougua magonjwa
ya akili lakini bado wako majumbani.
Bw.Kakoyo
alisema kuwa hadi sasa ni wagonjwa 792
ndiyo waliyotambuliwa kimkoa,Mbamba – Bay,Mbinga , Namtumbo,Songea Vijijini,
ambapo tafiti zimefanyika na kuwapata wagonjwa kuwanzishiwa matibabu.
Aidha alisema ubongo wa binadamu unahitaji
msaada mkubwa sana
wa ushauri nasaha,alisema katika kituo chao kitu cha kwanza wakimpata mgonjwa
wa akili wanampiga na maji, na kumpa ushauri nasaha ili ajue kuwa yupo salama.
Alisema watu wenye nia mbaya na watu
wengine wanaweza kuutumia ubongo wa mtu mwingine kwa lengo baya,na kumfanya mtu
yule akawa kama mtumwa wake akamtumia vile
anavyo taka.
Kuhusu kituo chake alisema kuwa anategemea
kupata watoto 30 mwaka ujao ambao wana matatizo ya akili,alisema pamoja na
asasi yake kujishughulisha na magonjwa ya akili lakini pia ametoa ushauri na
saha kwa mabinti wawili yatima.
Kufuatia ushauri huo mabinti hao sasa
wanasoma elimu ya juu,ambapo mmoja amehifadhiwa anasoma mwaka wa pili Chuo
Kikuu Mtwara tawi la SAUT,na wapili anasoma chuo kikuu cha ushirika Moshi.
RUVUMA MENTAL DISABILITIES ( RUMED)
wanapata msaada kutoka wa The Foundation for Civil Society .
Bwana Kakoyo alianza utafiti kwa watu wenye magonjwa ya akili mwaka
2001 Wilayani Mbinga,mwaka 2006 alifanya utambulisho wa asasi yake na mwaka
2007 hadi 2009 ikafika hadi Wilayani kuanzia hapo Asasi hii ipo katika viwanja
vya Sabasaba Matarawe mkoani Ruvuma
ndiyo makao makuu yalipo.
Monday, October 17, 2011
ELIMU YA WATU WAZIMA NI ELIMU YA KILA MMOJA WETU BWANA MPANGALA NA BI MWOMBEKI WAMESHUHUDIA HILO WALIPO JIFUNZA VITU WASIVYO VIJUA
Afisa elimu vielelezo Bi. Rose Mwombeki wa Manispaa ya SONGEA akiwa ofisi za TUJIFUNZE ni ofisi yake pia kwa sababu afisa huyu yupo katika Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima.
Bwana Mpangala Afisaelimu kilimo wa Manispaa ya SONGEA alitembelea ofisi ya TUJIFUNZE kujifunza mambo mapya.
Bw.Mpangala
Bi. Mwombeki
Maafisa hao wapo Paste Up Room wakipata maelezo ya Light table inayo tumika kuandaa kazi
Wanapata maelezo namna mashine hizo za uchapaji zinzvyo fanya kazi.
MAAFISA ELIMU VIELELEZO NA KILIMO WA HALMASHAURI YA MANISPAA YA SONGEA WATEMBELEA OFISI YA TUJIFUNZE KUJIFUNZA
Mhariri wa TUJIFUNZE Bwana Christian Sikapundwa mwenye suti ya zambarao akiwaonyesha wageni maafisa Elimu Kilimo Bwana Honoratus Mpangala mwenye kaunda suti mikono mifupi na Afisa Vielelezo Bi- Rose Mwombeki,Mahazeti ya kisomo ya Kanda zote saba ambavyo vilikuwa vikichapa.
Bi - Rose Mwombeki Afisaelimu Vielelezo Manispaa ya Songea
Bwana Honoratus Mpangala Afisaelimu Kilimo wa Manispaa ya Songea walitembelea TUJIFUNZE leo
Fundi mchapaji wa mashine Kubwa SORK Bwana Winifredy kaimbe akiwaonyesha wageni hao jinsi mashine hiyo inavyofanya kazi.
Bi.Rose Mwombeki Afisaelimu Vielelezo akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya TUJIFUNZE leo kabla ya kutembezwa kiwandani.
Mhariri msaidizi wa TUJIFUNZE Bwana Juma Nyumayo wa kwanza mwenye shati nyeupe akielezea maandalizi ya kuandaa Gazeti la TUJIFUNZE kwa ajili ya miaka 50 ya UHURU
Wageni bado wanapata maelezo jinso Elimu ya Watu Wazima ilivyo kuwa ikichapisha Magazeti hayo ya Vijijini, mezani ni nakala za magazeti hayo ya Kanda za Elimu .
Bwana Sikapundwa akiwaonyesha picha za Maafisa vielelezo wa Kanda ya Kusini
Wageni waipata maelezo ya mitambo ya uchapaji iliyopelekwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa ajili ya kuchapisha Magazeti ya Wizara na kusambazwa kwa wananchi mjini na vijijini.
Saturday, October 15, 2011
ADHABU YA KUWAFUKUZA MADIWANI WAKE WATANO UNACHAMA WACCM WA UKOSEFU WA MAADILI WAFUTWA
Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Bwana Emmanuel Mteming'ombe wakati wa mchakato wa kunadi wagombea wa Ubunge na Udiwani.
Mtahiki Meya wa Manispaa ya Songea Bwana Charles Mhagama wakati akijinadi wakati wa kuwania Udiwani katika Manispaa ya Songea ambaye baadhi ya Madiwani wa CCM na Wapinzani waliwanya fujo wakati wakimchagua katika wadhifa huo aliokuwa nao sasa,ingawa bado baadhi hawautambui wadhifa wake.
Mtahiki Meya wa Manispaa ya Songea Bwana Charles Mhagama wakati akijinadi wakati wa kuwania Udiwani katika Manispaa ya Songea ambaye baadhi ya Madiwani wa CCM na Wapinzani waliwanya fujo wakati wakimchagua katika wadhifa huo aliokuwa nao sasa,ingawa bado baadhi hawautambui wadhifa wake.
KAMATI ya Siasa ya
Halmashuri kuu ya Mkoa Mkoani Ruvuma
kupitia kikao chake kilichokaa hivi karibuni kimefuta adhabu ya
kuwafukuza uanachama Madiwani watano wa Chama Hicho kutokana na kile kilichodaiwa
ukosefu wa maadili wakati wa kumchagua Meya wa Manispaa hiyo.
Kwa mujibu wa Katibu
Mkuu wa CCM Mkoa wa Ruvuma Bwana Emmanuel Mteming’ombe baada ya kupitia maelezo
yaliyotolewa na Kamati ya siasa ya Wilaya ya kuwafukuza Madiwani hao,maelezo ya
uteuzi wa Madiwani waliyofukuzwa uanachama na Kamati ya Siasa ya Wilaya,Kamati
ya Mkoa imetengua uamuzi huo wa kuwafukuza madiwani hao uanachama. Na kuendelea
na uanachama na udiwani wao kama mwanzo.
Aidha Chama Cha
Mapinduzi ( CCM ) Mkoa kimesikitishwa sana na vurugu na fujo zilizojitokeza
katika Baraza la Madiwani wa kuchagua Meya wa Manispaa hiyo ,kufuatia vurugu
hizo Chama Cha Mapinduzi Kimekemea na kulaani tabia hiyo ya kufanya vurugu
katika vikao ambazo ni kinyume na kanuni za vikao na si tabia ya viongozi
wanaotokana na CCM.
Bwana Mteming’ombe alisema
kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa
kimeamua kutoa semina kwa Madiwani wote wanaotokana na chama hicho ili
kuwaelimisha weledi juu ya kusimamia utekelezaji mzuri katika Halmashauri zao.
Pamoja na mambo
mengine hali tete ya Baadhi ya Madiwani bila kujali Itikadi zao bado
wanashikilia hali ya kutomtambua Meya wa Halmashauri hiyo Mstahiki Meya Charles
Mhagama wa CCM Mbele ya Mkuu wa Moa huo alipokuwa akikagua shughuli za
maendeleo katika Manispaa hiyo.
MKUU WA MKOA WA RUVUMA AFUNGUA KIKAO CHA WADAU WA HABARI NA WAANDISHI WA HABARI SONGEA
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu akiwa Ofisini kwake akizungumza na waandishi wa habari wa Mkoa huo,leo amezungumza na wadau wa Habari na Waandishi wa habari katika ukumbi wa CWT katika Manispaa ya Songea.
Katibu Mkuu wa Ruvuma Press Club aliyesika karatasi akiwa na mdau wa Habari Bibi Mwenda wa wanza mwenye suti ya mistari kabla ya kikao kuanza.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakisubiri kikao kuanza na kutuma habari kwenye vyombo vyao wanavyo viandikia.
Bibi Joyce Joliga mwandishi wa habari mwenye suti ya zambarao nyepesi wakibadilishana mawazo na Bibi mdau wa habari na mjumbe wa kamati ya Maadili Katika Club ya Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa huo.
MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu afungua kikao
cha siku moja cha wadau wa Habari na waandishi wa Habari leo katika ukumbi wa
CWT katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
Bw. Mwambungu amewataka wadau wa habari utoa habari kwa
waandishi wa habari kwani bila ushirikiano wao na waandishi wa habari wananchi
watakosa habari ambazo ni haki yao
kuzielewa.
Aidha na waandishi wa habari nao wanawajibika kufuata maadili
ya kazi yao ya
kuandika habari bila kuegemea upande mmoja,ambazo haziwezi kuumiza mtu au
kumnufaisha mtu kwa matakwa yake.
Kikao hicho kimejumuisha waandishi wa mkoa wote wa Ruvuma na wadau kadhaa kutoka katika Manispaa ya Songea.
Subscribe to:
Posts (Atom)