Tuesday, July 26, 2011

SIKU YA MASHUJAA KITAIFA IMEFANYIKA MKOANI MTWARA NA MGENI RASMI NI RAIS JAKAYA KIKWETE NA KUTEMBELEA CHUO CHA VETA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete jana alikuwa mgeni rasmi katika siku ya mashujaa mkoani Mtwara na leo,ametembela chuo cha VETA na kituo cha kilimo cha Naliendele mkoani humo na kuzungumza na wananchi.
Mwananchuo wa VETA mkoani Mtwara anaiomba serikali iwaajiri vijana wanao maliza katika vyuo vya VETA nchini.

MAAJABU YA VIUMBE HAI HASA MCHWA NA MAAJABU YAKE YA KUJENGA VICHUGUU VIREFU KAMA ROSHENI

 Mchwa ni wadudu wadogo lakini ni wajenzi wa hali ya juu kabisa kwa kutumia mimea wanayokula katika ujenzi wa vichuguu,kutokana na utafiti imeripotiwa kuwa kuna vichuguu vyenye urefu wa maili mbili kwenda juu ni sawa na urefu wa nyumba ya rosheni inayojengwa na mainjinia waliyosomea kazi hiyo.
 hivyo ni baadha ya vichuguu vilivyo jengwa ba wadudu hao kwa kutumia mazingira wanayoishi.
Hiki nacho ni kichuguu kinaonekana kama uyoga  ama kibanda cha kuhifadhia chakula kwa baadhi ya makabila ya kiafrika hujenga hivyo kwa lengo la kuhifadhi chakula chao kwa ajili ya matumizi ya baadaye.

WAKATI MKOA WA DODOMA NA BAADHI YAKE NCHINI INA UHABA WA CHAKULA,MKOA WA RUVUMA MAHINDI YA MWAKA JANA NA YA MWAKA HUU YANA KUTANA GHALANI

Waziri wa kilimo na chakula  Profesa Jumanne Maghembe akiwakilisha bajeti ya wizara hiyo,amakumbana na changamoto lukuki kutoka kwa waheshimiwa wabunge ,wakitetea wakulima jinsi wanavyo pata shida katika kuyauza mazao yao kwa kukosa soko la uhakika yakiwemo,Mahindi,pamba,tumbaku,kahawa,chai,ndisi,tangawizi,Na mengine mengi.
Aidha ukosefu wa chakula cha kutosha katika mikoa ya Dodoma na mingine nchini,wakati mkoa wa Ruvuma mahindi yamerundikana ya mwaka jana na mwaka huu ambayo yanasafirishwa nje ya mkoa huo kila kukicha.

Tuesday, July 19, 2011

ELIMU HAINA MWISHO NI GAZETI LA KISOMO KANDA YA ZIWA MWANZA AMBALO HUSOMWA WANANCHI WOWOTE

Magazeti hayo ya kisomo ya Elimu Haina Mwisho Kanda ya ziwa Mwanza na TUJIFUNZE KANDA YA KUSINI songea ni mpango wa serikali wa kuchapisha kwa ajili ya wanajisomo wa kujiendeleza,wakati wakijifunza kuandika,kuhesabu na kusoma KKK lakini cha ajabu leo kuna baadhi ya watu wanabeza elimu ya watu wazima.
Cha kushukuru Serikali imeliona hilo imeanzisha upywa Kurugenzi yake na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi Bwana Salum Mnjagila ambaye ni mwana - kisomo halisi,akiwezeshwa hadhi ya Elimu ya Watu Wazima  na Nje ya Mfumo Rasmi itarudi kupitia mipango ya MUKEJA,VICOBA NA MEMKWA

KANDA ZA KUSINI NA ZIWA ZIMECHAPA MAGAZETI YA KISOMO ZAIDI YA 1000 NA KUYASAMBAZA

 Katika jitihada za kuwafikishia wananchi wa kisomo katika madarasa yao ya kisomo ya Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmi,Kanda ya Kusini yenye mikoa ya Mtwara,Lindi na Ruvuma ambapo kituo cha Uchaoaji cha Kanda kilipo kilianza kuchapisha magazeti ya TUJIFUNZE  kama yanavyo onekana matoleo Na1 Agosti 2009 na toleo Na 2 Desemba 2009.
 Likafuatia Toleo Na.3 Januari 2010
Hatimaye Toleo Na 4 Mei 2010,na matoleo mengine katika Baadhi ya halmashauri zilitaka kuchapisha machapisho yao ya mafunzo juu ya ahtari ya virusi vya UKIMWI na ugonjwa wa UKIMWI halmashauri za Wilaya ya Songea Manispaa na Mbinga.
Katika maelezo ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt Shukuru Kawambwa amesema Wizara yake imeweka malengo ya Uchapishaji wa magazeti hayo katika Kanda zake zote saba.Kutokana na Gazeti hilo ndipo Blog ya TUJIFUNZE KUSINI ikazaliwa kwa lengo la kutoa habari za kusini mwa - Tanzania na maeneo mengine nchini na nje ya nchi.

Bajeti ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi kuanza leo,malengo kadhaa kutajwa.

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mke.Dkt Shukuru kawambwa katika mhtasari wake wa bajeti ya wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi umeelezea utekelezaji wa malengo ya sekta ya elimu mwaka 2010 na 2011 na malengo ya mwaka 2011 na 2012.
Baadhi ya malengo aliyoyataja ni pamoja na Halmashauri 16 nchini zimetoa chakula cha mchana katika shule za msingi,kutoa mafunzo kwa walimu wa masomo ya sayansi na TEHAM,hesabati.
katika elimu ya watu wazima na nje ya mfumo rasmi imeweza kusambaza vitabu vya kufundishia na kujifunzia katika vituo vya MUKEJA na kuchapisho ya Mpango wa ndiyo naweza katika halmashauri 6 za majaribio katika kufundisha watu kusoma,kuandika na kuhesabu kwa njia ya TVna Radio

Saturday, July 16, 2011

JUMAMOSI YA LEO MJINI SONGEA HALI YA UMEME IMERUDIA HALI YAKE YA KAWAIDA YA MGAO , NA USAFI NAO BADO NI TATIZO HASA UZOAJIWA WATAKA

Hiiyo ni hali halisi ya Blog hii ilivyo kuta uchafu ulivyo achwa katika guba hilo la kuhifadhia taka kwa muda kisha magari ya Halmashauri ufika na kuyazoa kwenda kuyatupa eneo maalumu na kuyachoma moto.
Hakika taka hizo ni karaha kwa wakazi wa eneo la taka hizo,baaya pombe,mashine za kukoboa mpunga na kukoboa mahindi na kusaga unga.ni kweli zinakera,zinatoa harufu mbaya na kali ambayo kiafya si nzuri kwa maisha ya binadamu.Uchafu kama huo usiyo zolewa kwa muda mrefu omeenea katika maguba yake katika halmashauri hii ya Songea.

Friday, July 15, 2011

UMEME UMESABABISHA WAKAZI WA SONGEA NA VITONGOJI VYAKE KUKOSA HUDUMA ZA KIBENKI LEO

 Umeme imekuwa gumzo leo mjini hapa,wengine wanasema huwenda mashine za kuzalisha umeme zimekufa,lakini wengine wanasema labda mafuta huwenda hakuna ,lakini mmoja ndiyo alitoa mpya kuwa mwenye kuleta mafuta katika mitambo ya kuzalisha umeme hulo kiblang'oma Manispaa ya Songea hajalipwa pesa yake.
Yote tisa lakini watu wapo mlangoni wakisubiri miujiza umeme uwake huduma za benki ziendelee,maana kila mmoja alikuwa na shida yake ya kutatua baada ya kupata pesa au kuweka pesa mahala pa usalama ambapo bila umeme kuzipata pesa hizo ni shughuli.
 Nishati hizi za umeme hapa mkoani Ruvuma ilikuwa ni kitu kidogo sana,kwani vyanzo vya upatikanaji wake ni rahisi mmno iwapo serikali ingevutia wawekezaji katika nishati ya umeme.Kuna maporomoko ya nakatuta yenye uwezo wa kuzlisha umeme,kuna makaa ya mawe yenye uwezo wa kuzalisha umeme isitoshe tuna Urenium namtumbo yote hayo yangeweza kuzalisha umeme wa uhakika,hata wenye Grid ya Taifa wasingfua dafu,Lakini yangoswe ni mwachie ngoswe mwenyewe,yetu ni kushuhudia jinsi nishati ya umeme isipopewa kipaumbele,Humo ni ndani ya Benki,unayoyaona ni Computer hizo,haziwezi kufanya kazi bila ya umeme je mfanyakazi akae mbele ya computer iliyo giza atamhudumia mteja?
 Hivyo hivyo kwenye ATM ni mtandao wa computer pia bila umeme huwezi kutoa pesa humo kwenye kisanduku hicho wao wajanja wanakiita ATM basi mradi wenye kushika tama,baki wenye kushika vichwa nao hivyohivyo pesa hakuna,kuna wenye wagonjwa hospitali wameambiwa wakanunue dawa,wengine wameambiwa wawe na shilingi 2,000/= za kumwona mgangaili amwandikie dawa akanunue maduka ya mitaani.Umeme huu jamani utaumbua watu kweli.Shida haina ujanja,lakini tutafika,wakati wenzetu wanapeta na umeme wa Grid ya Taifa Ruvuma tunavuma kwa kilimo,umeme wa mafuta anayoletwa kwa malori,Hivyo ni lini na wana - Ruvuma nao watakuwa na umeme wa uhakika?
 Nisiseme mengi mengine yanajieleza ukiziona picha hizo,ni jinsi gani wapiga kura hawa wanavyo kosa huduma muhimu.
Ni kawaida lakini kawaida haizoeleki hata chembe,wengine wanapeta kwa umeme wa Grid na wengine wanambulia Diesel ili mtambo uzalishe umeme unategemea nini,nakama Jenereta lenyewe ni la enzi ya Nuhu ni kila kukicha ICU.

Thursday, July 14, 2011

MITANADO YA PUBLISHING INAVYO FANYA KAZI PAMOJA

 Huwezi kuwa na Internet Blog,twitter na mitandao kadhaa bila ya kuwa na Computer
 Huwezi kusoma magazeti,majarida,vipeperushi bila ya kuwa na mitambo ya uchapishaji
Hivyo ndivyo mitambo midogo inavyofanya kazi ya kuchapisha machapisho mbalimbali yakiwemo kagazeti.TUJIFUNZE Kanda ya Kusini hatuvumi lakini tupo pamoja

POSHO YA MIITO YA USIKU YA SHILINGI 10,000 KWA MADAKTARI NCHI HAITOSHI NDIYO INAWAFANYA KUFANYA KAZI ZA ZIADA

Viongozi wa Chama cha Madktari Nchini wasema tangu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamiikuingia madarakani hajawahi kukutana na Viongozi wa Chama cha Madaktari nchini kuzungumzia matatizo lukuki yanayo ikabili Sekta ya afya nchini. Hivyo ni juu ya waziri huyo kukutana na viongozi hao wanaweza kuwa na jambo la kuleta tija katika sekta ya afya japo wa nusu saa hivi atapata kitu cha muhimu kutoka kwa Madaktari viongozi hao.
Viongozi hao wanasema wanaipenda sana kazi yao kwa kuwa wamesomeshwa na Serikali yao,ila maslahi hayaendi na elimu waliyokuwa nayo,mazingira ya kufanyia kazi hayafanani ha elimu waliyo nayo.wametoa mfano wa posho inayotolewa ya miito ya usiku kwa Daktari bingwa ya shilingi 10,000/= kwa wakati wa leo haimsaidii daktari huyo.Maana hana usafiri labda adandie daladala toka Mbagala hadi Mhimbili,au akodi gara kwenda na kurudi hiyo 10,000/= bado ipo?

Lazima serikali kupitia Wizara ya Afya iwe na jicho la kuliona hilo,Zahanati nyingi zimejengwa kwa nguvu ya wananchi lakini hazina waganga,madawa,nyumba za waganga wenyewe au wahudumu.Bado kunachangamoto nyingi Wizara ya afya.

ROSTAM ALIZA WAPIGA KURA WAKE WA JIMBO LA IGUNGA JANA

 Wananchi wa jimbo la Igunga jana hawakuamini kasikio yao waliposikia Mhe.Rostam Aziz akisema kuwa pamoja na kafanikio yote yaliyo patikana katika miaka yake ya Ubunge Jimboni humo, yakiwemo ya Elimu ,Afya na maji,sasa inatosha kwa kutoka moyoni mwake alisema anajiuzuru,Ujumbe wa NEC CCM na Ubunge.Ukweli wengi walilia toka moyoni mwao kutokana na yale Mhe. Aziz aliyoyafanya ya kupeleka maendeleo katika Jimbo hilo.Maana imekuwa kwa wa - Tanzania wengi kuwa wanafiki wa kujifanya wanalia kumbe wanasema afadhali achie ngazi ili hali ya Igunga iwe kama alivyoikuta,kwa kuwa uwezo wa kuifanya Igunga ya maendeleo hawatakuwa nao.Aziz hategemei fedha za Ubunge kuendeleza Igunga bali ni pamoja na fedha ndani ya familia yake ndizo zilizofanya Igunga ya leo.
 Lakini naye Kaimu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. John Joel anasema kuwa huo ni uvumi kwani Bunge halijapata habari za Mhe. Aziz kujiuzuru kwake.
Je kuhusu tukio hili la Mwana CCM kujivua katika madaraka yake,Bw.John Chiligati atasema nini ?

Kwa kawaida mtu napowafanyia watu maendeleo kwa faida yao siyo yake ni vyema kumshukuru wangapi matajiri nchi hii,wamefanya maendeleo katika maeneo yao licha yakuwa wao si wabunge wala wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM.Kwa kauli yake Mhe. Aziz Jana alisema "napisha marumbano ndani ya Chama changu na Vyama vingine yasiyo niletea faida katika maisha yangu" hiyo tu inatosha kuona ni jinsi gani binadamu alivyo na macho ya kuona kwa muda mfupi mambo mazuri na baadaya macho hayo hayo hayaoni tena jitihada za mtu yule yule aliyefanya mapindizi katika maendeleo  ya mahali husika au ya watu kadhaa nchini.Je hiyo ndiyo fadhila ya watu wanaojitoa mhanga katika kuwaletea maendeleo wananchi? au ndiyo tusema wamevaa miwani ya mbao yasiyoweza kupisha ukweli wa mambo?.

Sijui,tunashabikia lakini ukweli unabakia palepale mwenye uwezo ndiye atakaye saidia kuleta maendeleo,na asiye na uwezo atabakia kusema na kuwasema wenye uwezo,ndicho alicho nacho.Hii nakataa katu pesa ya ubunge wako bila ya miradi yako uliyokuwa nayo kabla ya kuingia jengoni ,halafu upeleke maendeleo katika jimbo lako mbona hiyo ni ndoto,Akina Aziz hao wako wengi wakiamua kufuata maelekezo yaliyotolewa ya kuachia ngazi waliyokuwamo jengoni matokeo yake mtayaona.Ingawa ni mabingwa wa kushabikia mambo.

Saturday, July 9, 2011

BREAKING NEWS ! ! ! ! HAYAWI HAYAWI LEO YAMEKUWA SUDANI KUSINI LEO JAMHURI KAMILI

Mfanya biashara wa kimasai Mtaznaia akiuza dawa zake Sudani ya kusini,na wenzake kutoka nchini Kenya wakifanya bishara ya nguo nchini humo

IBADA YA KUMKUMBUKA MAREHEMU CHIHOMO SOKONI NYUMBANI KWAKE NA PADRE JOHN MAPUNDA WA KANISA LA MT.NICOLAU ANGLICANA SONGEA MJINI LEO

 Padre John Mapunda wa kanisa la Aglican la Mtakatifu Nicolau Songea Mjini akisoma misa ya kumkumbuka marehemu Chihomo Sokoni aliye fariki Ijumaa kuu tarehe 22/4/2011 na kuzikwa tarehe 23/4/2011 siku ya mkesha wa Pasaka.
 Padre Mapunda akiongoza ibada ya kumkumbuka marehemu Chihomo Sokoni
 Mke wa marehemu Chihomo Sokoni Bibi Tarsisia Milinga wa katikati amepiga magoti tayari kwa kula mkate na divai.
 Bibi Tarsisia amesha pewa mkate na divai na Padre John Mapunda
 Picha ya Bibi Tarsisia Milinga ya kumkumbuka mpendwa mme wake kwenye fremu nyumbani kwao.
 Picha ya pamoja ya familia ya Bibi Tarsisia Milinga  mara baada ya ibada ya kumkumbuka marehemu mkwe wao Sokoni nyumbani kwa marehemu leo.
 Mtoto wa nne wa marehemu Chihomo Sokoni Sunday Sokoni kidato cha sita Jijini Dar es salaam alifika kwenye arobaini ya Baba yao mpendwa. mjini Songea leo.
 Kwaya iliimba nyimbo za maombolezo,na za tenzi za Rohoni na za kutukuza Mungu wakati wa Ibada hiyo
 Sifa na utukufu ilikuwa ndiyo neno la kutiliwa mkazo kuwa Mungu amewapenda wanadamu na kuwalete mkombozi Yesu Kristu na amuaminiae ataokoka,na kila anayeomba kwa jina lake atapewa.
Picha ya pamoja ya Mama wa marehemu  Sofia Kayanja na mke wa marehemu Tarsisia Milinga. mwenye nguo nyeupe.

FAMILIA YA MAREHEMU CHIHOMO SOKONI LEO IMEWASHUKURU MAPADRE,MADAKTARI NARAFIKI WA MAREHEMU CHIHOMO SOKONI KWA KUSHIRIKI KATIKA IBADA YA KUMBUKUMBU LEO MJINI SONGEA

Familia ya  Mama Sofia Kayanji Sokoni wa Manispaa ya Songea leo imefanya Ibada ya kumbumbu ya Mtoto wao Mpendwa Chihomo Sokoni aliyefariki Ijumaa kuu mwaka huu tarehe 22/4/2011 na kuzikwa siku ya mkesha wa sikukuu ya Pasaka tarehe 23/4/2011,familia hiyo imewashukuru Mapadre,waganga,majirani,marafiki wa karibu na Marehemu,na wote wenye mapenzi mema waliyoshiriki wakati wa kuugua,mazishi na hatimaye leo 40 na ibada yake ya shukrani kwa Mungu.Roho ya Marehemu Chihomo Sokoni ikae mahali pema peponi Amina.
 Mama Sofia Kayanja Sokoni akiwa pamoja na wote waliofika katika ibada hiyo iliyoongozwa na Padre John Mapunda wa Kanisa la Anglican Songea Mjini Leo.
 Mpendwa Mke wa marehemu Chihomo Sokoni Bibi Tarsisia Milinga akiwa bado na majonzi ya kuondokewa na Mumewe Mpendwa,lakini sisi kama binadamu kazi ya Mungu haina makosa ,Marehemu Chihomo Sokoni Mungu alimpenda zaidi,akamchukua,basi njia hiyo ni kwa kila mmoja wetu ataipitia.Pole sana kwa yote yaliyotokea.
 Watoto , wa marehemu,mama na ndugu wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ibada ya kumbukumbu ya Marehemu Baba yao mpendwa Sokoni.
 Mjomba wa marehemu Chihomo Sokoni Daktari mstaafu Philipo Kayanja
 Mdogo wa Marehemu Bwana Amani Sokoni
 Mdogo wa Marehemu Chihomo Sokoni Bwana Yohani Sokoni
 Shemeji wa marehemu Chihomo sokoni Bwana Milinga wa Peramiho.
picha ya pamoja ya watoto wa marehemu na mama yao.yaha hapo chini.