Sunday, March 31, 2013

WAENDESHA BAISKELI WAWE MAKINI WANAPOINGIA BARABARA KUU,ILI KUEPUSHA AJALI KAMA MWENDESHA BAISKELI ALIVYO GONGWA NA PIKIPIKI LEO MJINI SONGEA BAADA YA IBADA YA PASAKA

 Mwendesha baiskeli aliyegongwa na pikipiki leo Mjini Songea
Baadhi ya watu waliyomsogeza mwendesha baiskeli huyo
Mjini kusitokee kitu watu hujaa kushudia tukio.


AJALI ya baiskeli kugongwa na pikipiki katika makutano ya barabara ya Sovi,Polisi katika Manispaa ya Songea iliyotokea leo baada ya mwendesha baiskkeli huyo kuingia barabara kuu bila kusimama na kuangalia pande zote hatimaye kugongwa na pikipiki iliyotokea kona ya Sovi.
Baada ya mwendesha pikipiki kumgonga mendesha baiskeli huyo ambaye jina lake halikutambulika mara moja,wote walianguka kila mmoja na wakati wake.
Mendesha pikipiki alitaka kukimbia,lakini wasamaliam wema walimsihi aende polisi kuelezea tukio hilo,ambapo mwendesha baiskeli alipoambiwa kupelekwa hospitali kwa matibabu alikataa kwa kuogopa hatia kutokana na kuvunja sheria za usalama barabarani.
Kwa hiyo siku kama hizi za sikukuu,watu wanatakiwa kuwa makini katika uendeshaji wa vyombo vya moto na baiskeli kuwa maakini.

No comments:

Post a Comment