Saturday, March 9, 2013

UHURU KENYATTA AWASHUKURU WA KENYA KWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIGA KURA

 Uhuru Muigai Kenyatta ashinda kiti cha urais kwa kupata kura 6,173,433 sawa na asilimia 50.07% na kukabidhiwa cheti cha ushindi wa Urais  na mwenye kiti wa Tume ya uchaguzi IEBC Mhe.Issack Hassan,na ataapishwa baada ya siku 14 kulingana na Katiba mpya ya Kenya ya mwaka 2010.
Rais Mteule wa Jamhuri ya Kenya Mhe.Uhuru Muigai Kenyatta,amekabidhiwa cheti cha ushidi wa Urais kufuatia ushindi aliyoupata kwa kura 6,173,433 sawa na asilimia 50.07%  na kumwacha kwa mbali Bw.Raila Odinga kwa kura 5,340,536


RAIS mteule wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Muigai Kenyatta, amewashukuru wakenya wote kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa kwanza wa kihistoria ambao umechukua muda mrefu chini ya  Katiba mpya  ya mwaka 2010.
Mheshimiwa Kenyatta alisema hayo leo katika ukumbi wa chuo kikuu cha kikatoliki cha Afrika mashariki baada ya kukabidhiwa cheti cha ushindi  wa kiti cha Urais kwa kura 6,173,433 sawa na asilimia 50.07% na mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi IEBC Bw.Issack Hassan.kwamba wamevumilia jua, wametumia muda mwingi hadi kufikia nia yao ya kuwapata viongozi wa kuiongoza Kenya.na kujitokeza kwa wingi katika kupiga kura.
Aidha alisema ushindi uliopatikana siyo wa Jubilee peke yake bali ni kwa wakenya wote,na kwamba ushirikiano wao ndiyo  utaofanya serikali ya Kenya ipige hatua katika maendeleo,pia kudumisha amani na utulivu uliyojitokeza wakati wa uchaguzi wa viongozi waliowachagua wenyewe.
Alimewashukuru Tume ya uchaguzi IEBC,wachunguzi wa nje na ndani ya nchi,vyombo vya habari kwa kazi kubwa waliofanya tangu siku ya kupiga kura,kuhesabu hadi kutangazwa kwa matokeo.
Alisema katika chaguzi za nyuma vyombo vya habari viliwajengea wananchi chuki tofauti na uchaguzi huo,ambao unaingia katika kitabu cha kihistoria ya Kenya kufanya uchaguzi wa amani na utulivu ambapo Dunia ilikuwa na wasiwasi wa kutokea machafuko wakati wa upigaji wa kura,kuhesabu hadi kutangazwa kwa matokeo.
Uhuru Kenyatta amewahakikishia wakenya kuwa atatimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni zake,katika kuinua uchumi,amani na utulivu miongoni mwa wakenya milioni 40,na kwamba amemshukuru Mungu katika kufanikisha uchaguzi huo kwa kufanyika kwa amani na utulivu.

No comments:

Post a Comment