Thursday, March 14, 2013

KIKUNDI CHA SANAA CHA FATAKI NI MUHIMU SANA KATIKA JAMII YETU

Kikundi cha Fataki kinacho rushwa na TBC, ni kikundi muhimu sana kwa kuielimisha  na kuikosoa Jamii.,Ukipata muda kama upo Tanzania Kifuatilie,hasa wanafunzi wanaochukua Lugha ya Kiswahili.
 Wahenga walisema kuwa hata njinga huwa anatoa wazo litakalo msaidia mjanja.
 Wengi wetu tunazema ni mchezo wa kuigiza,hata kama ni wa kuigiza,je ujumbe wake ukoje kwa Jamii ya Kitanzania? Maadili yamemomonyoka miongoni mwa vijana, haiyamkini hata watu wazima ambao wanaiga mambo bila ya kuchuja madhara yake kwa Jamii.


Kikundi cha sanaa cha Fataki ambacho kinarushwa na TBC kina umuhimu mkubwa kwa jamii yetu ya Tanzania hasa wakati huu ambao jamii inashangaa kuona vikundi vinavyoibuka kila kukicha vinafanya mambo ambayo Jamii yetu ya Kitanzania  na Kiafirika haijawahi kufanya.

Kikundi hiki nasema ni muhimu kwakuwa ,wanaikosoa,wanaelimisha,wanaitahadharisha na wanaiburudhisha Jamii kwa kupitia Fasihi Simulizi,ambamo ndani yake kuna Maudhui,Ujumbe,Fasihi,Misemo,Methali pamoja na Vivumishi,ambavyo Mwanafasihi akikifuatikila kipindi hicho anaweza akaandika kitabu cha fasihi  ambayo itasaidia kwenye kukuza Lugha yetu ya Kiswahili.

Hasa vijana wanaosoma wangejaribu kukifuatilia kipindi hicho kinachorushwa na TBC, ninaimani,akirudi kusoma vitabu vya Fasihi ( Fasihi andishi ) hatapata shida kubwa katika kuchambua Fasihi na Kumchambua Mwandishi wa Fasihi hiyo.

Tatizo vijana wetu hawana muda wa kuangalia Tamthilia kama zile,huwenda wakidai wanakikundi taaluma yao ni ndogo,lakini tukumbuke Lugha haina elimu, elimu itaongezeka ukienda shule ambako utaenda kuiboresha ili upate Lugha fasaha.

Pia Fasihi simulizi ilianza kabla hata maandishi hayajaanzwa,ilikuwa kwenye unyago,jando, sherehe na misiba.Ndiyo maana kwenye sherehe nyimbo na ngoma zina pigwa na kuimbwa,hali kadhalika kwenye misiba watu wanaimba nyimbo za kuomboleza na hata kucheza kwa baadhi ya makabila.

Leo nimevutiwa na kikundi hicho pale walipotamba na kumsihi kijana ambaye alishika upanga kwenda kupambana na watu ambao wamechinja ,kwake yeye mnyama aliye chinjwa na watu hao yeye hawezi kula,maana yeye ndiye aliyekabidhiwa kisu kuchinja,lakini wazee walimpa darasa na akaelewa kuwa alicho taka kukifanya hakiipendezeshi Jamii.

 ‘ Babu zetu walikuwa wakichinja lakini kila watu walikuwa wakiabudu vitu ambavyo katika ibada zao wa alikuwa wanajua wanampendezesha Mungu,Dini hizi zimeletwa tu hatukuwa nazo, kwanini tuifukuze Amani nchini kwetu kwa ajili ya Dini zilizoletwa” alisema mzee mmoja.

No comments:

Post a Comment