Askofu Mkuu Dkt Norbert Mtega akibariki waumini baada ya Ibada ya PASAKA Kanisa kuu la Songea leo.
Waumini wakiwa katika Ibada ya PASAKA
Waumini
Kwaya ya DONBOSCO ambayo imekoleza ibada hiyo leo siku ya PASAKA
Zifuatazo ni picha za umoja wa Wanamama Katoliki ( WAWATA) ,Wa Jimbo la Songea
Kutoa vipaji akina mama ( WAWATA)
Vipaji akina mama ( WAWATA )
Katika masomo ya Ibada ya PASAKA akina mama wa WAWATA wakipeleka Biblia ili kwenda kusoma na baadaye Injili.Aliyeshika Biblia menye gauni la kijani ni Bi. Cosensa Mbena na wa pili ni Bi Geni.
KATIKA Ibada ya PASAKA kwenye
kanisa kuu la Katholiki la Jimbo kuu la Songea
la Mt.Mathias Mulumba Kalemba mjini Songea,ambao waumini wa kanisa hilo waliungana na wenzao
Duniani kote kwa sherehe za PASAKA,
Hata hivyo alisema kuwa
nchi ya Tanzania
haikuwa na Historia ya umwagaji wa damu hata wakati wa kudai Uhuru wake,lakini
kuna baadhi ya raia wamemwaga damu kutoka kwa watu wasio eleweka.
Hayo yametolewa katika
mahubiri ya Askofu Mkuu wa Jimbo hilo,Dkt.Norbert Mtega katika Ibada ya sherehe
za PASAKA leo,na kwamba ukombozi wa Yesu Kristu kwa kufa na kufufuka kwake uwe
kwa watu wote wanao mwamini Mungu hata kama hawajabatizwa.
Aliwashukuru sana waandishi wa habari katika mchango wao wa kuandika na
kuripoti uharibifu na vifo kadhaa vilivyo jitokeza katika nchi yetu na
wengine kupata vilema vya kudumu kama vile kutolewa macho.
Alisema kuwa waumini waende
kumtangaza ufufuko wake wa amani,upendo
na mshikamano,bila ya kujali tofauti za Imani miongoni mwao,kwani wote ni wana
wa Mungu.
Aidha alisema kuwa waumini wanatakiwa
kuwa na Biblia mikononi mwao,nyumbani kwao na msalaba ambao ni ukombozi wao,kwani
Biblia ni neon la Mungu la uzima ,nasio kama vitabu vingine.na kwamba wanawake
wameonekana kuwa na mwamko wa kuwa na Biblia na kushiriki katika Jumuia
ndogondogo.
Amewataka wanaume nao
kushiriki katika uinjilishaji kwa kwenda kwenye Jumuiya ndogondogo ,pamoja na
Biblia kama wanavyo fanya wanawake,ambapo
Umoja wa Wanawake katoliki ( WAWATA ) Jimbo la Songea walitoa vipaji katiba
Ibada ya PASAKA.
No comments:
Post a Comment