Sunday, March 24, 2013

SIKUU YA MATAWI NI MWANZO WA WIKI YA MATESO YA YESU KRISTO ,LEO WAUMINI KATIKA KANISA LA JIMBO KUU LA SONGEA WAKIWA NA MATAWI WAKISHANGILA,WAKIIMBA HOSANA JUU MBINGUNI.

 Ndani ya kanisa kuu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba Mjini Songea wakishangilia kwa matawi,Jumapili ya Matawi wakuingana na waumini wengine Duniani kuadhimisha sikuu ya matawi.
 Reverent Father Otieni wa katikati aliyoendesha ibada hiyo takatifu,Pia ni Paroko msaidizi,akisubili vipaji.
 Waumini na mitende yao mikononi
 Waumini wa Jumuiya ya Mfaranyaki wakipeleka vipaji,Anayetoka ni Bwana Matembo fundi hodari wa saa. Mjini Songea.
 Wasichana wa sekondari ya wasichana Songea wakipeleka vipaji vyao

Wakipeleka vipaji

NI mwanzo wa juma kuu la mateso na kusulubishwa msalabani na siku ya tatu akafufuka.Mateso na kufa kwake msalabani ni kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu kwa dhambi zake. Kanisa linakaribia katika adhimisho la Juma la Pasaka Kabla ya Misa kulikuwa na maandamano ikiwa ni ukumbusho wa kuingia kwake Kristu kwa shangwe katika mji wa yerusalemu.Ambapo alipofika mlima ya mizeituni Yesu aliagiza wanafunzi wake wamletee mwana punda .Punda na mnyama mpole,pamoja na upole wake ,punda hutumiwa na watu maskini.ndiyo maana Yesu Kristu alipanda mwana Punda ili kuonyesha kujishusha kwa kupanda punda.Angewza kupanda farasi ambaye hutumiwa na watu maarufu na matajiri ila Bwana alijishusha na kupanda  mwana – punda.
Kwa hiyo kifo  na ufufuo wa Yesu Kristu kwa ajili yetu sisi  kunakofanywa  na umauti wa watu.Na iwapo watu  wakimsadiki yeye watapata uzima wa milele.Wamwaminiye na kumsadiki ambao  wamtangazae na kumuhubiri yeye , watakuwa wanamtangaza na kuihubili Injili kwa watu wote waliyokwisha kata tama ya maisha ya uzima wa milele   hivyo kwa kupitia kwao wataokolewa kwa jina la Yesu
Aidha  waumini wa kanisa hilo kote duniani wamefanya maandamano na matawi mikononi na kuimba Hosana,Mwana wa Daudi,ndiye mbarikiwa,yeye ajae kwa jina la Bwana,Mfalme wa Israeli ,Hosana juu mbinguni.

No comments:

Post a Comment