Wednesday, March 20, 2013

MATAPELI WASICHAFUE DINI ZA WATU KUIBIA WATU FEDHA ZAO,WEZI WA MOROGORO SASA WAMEHAMIA SONGEA WANAJIFANYA WACHUNGAJI AU MAPADRI WANAONUNUA MADINI

KIKUNDI cha matapeli wa Manispaa ya Morogoro wanaojifanya wanaulizia STAMICO na kisha wanajifanya wana  madini aina ya dhahabu ambayo ni dhahabu feki ni koki za maji za shaba zilizoyeyushwa na kuhifadhiwa kwenye vyupa vidogo,sasa wameingia Manispaa ya Songea.
Katika hali siyo ya kutegemea Mama mmoja mkazi wa manispaa ya Songea alikutana na dhahama hiyo,ambapo matapeli hao walimteka hadi Mkoani Njombe,ambako walimtaka Mama huyo akawape fedha milioni 50,ili wampe dhahabu ,Lakini dhambi mara nyingi huwa hazipenyi kwa mtu ambaye amatakasika .Matapeli walivyofika Njombe CRDB Benki walimwamuru mama yule akawachukulie fedha .

Mama alipokaribia mlango wa Benki alizinduka akapata akili ya kupiga simu Songea,matapeli walianza kumkaripia kuwa usiwasiliane na watu maana ni siri yetu wewe na sisi sasa unafanya nini,Roho ya amani ilimjia akaingia Benki ,peke yake,Tapeli wale walitawanyika hawakumfuata ndani ya Benki maana walijua dili imeharibika ,waliingia kwenye gari lao la kifahari.wakakimbia.

Uongozi wa CRDB Njombe ukawasiliana na polisi ambao walimchukua mama huyo na gari la polisi hadi Songea,kati ya  matapeli hao wanne mmoja alijifanya padre yeye ndiye mnunuzi wa madini kumbe tapeli.Kwanini hawa wanachafua Dini za watu kwa  kwa kujifanya mapadre ama wachungaji kwa ajili ya kuibia watu fedha zao? Habari ndiyo hiyo.

No comments:

Post a Comment