Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Norbet Mega Kwenye ibada ya Pasaka
Askofu Mtega akianzaIbada ya Alhamisi Kuu leo Mjini Songea
Askofu Mkuu Norbet Mtega akiwa Altareni
Askofu Mtega akitoa baraka
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Dkt Norbet Mtega akipokea vipaji siku ya Alhamisi kuu.
Mishumaa
ASKOFU Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbet Mtega
amelitahadhahaisha Taifa kuwa Ibilisi wamaingia nchini ili kulisambalatisha
taifa ambalo lina amani na ushirikiano wa wakazi ambao wanashirikiana kwa kila
jambo kutokana na mshikamano waliokuwa nao.
Askofu Mtega alisema Ibili ana njia nyingi za
kulisambalatisha taifa hilo,kwani
mambo yamekuwa yanazidi ya kutishia waumini wa madhehebu wa Dini ya Kikristo
waogope kwenda kuabudu kwenye nyumba za Ibada kwa ajili ya kumwogopa ibilisi ailiyoingia nchini.
Alisema Ibilisi hawafurahii,Uhuru,Muungano,Ushirikiano na
umoja tuliokuwa nao, bali wanataka kuturudisha katika utumwa, na kila mmoja
anaelewa athari za utumwa, hivyo utumwa huo unataka kurudi kama
si wao ni watoto wao au wajukuu wao.
Aidha alisema kuwa sumu inayoingia katika taifa kwa kupitia
ibilisi, ni adui wa Uhuru wetu,Muungano wetu,Ushirikiano wetu na mshikamano
wetu ambapo Wakristu na Waislamu walikuwa akishirikiana katika shida na raha
sasa Ibilisi anatumia njia zake kuusambaratisha umoja uliopo.
Alisema tuwaombee viongozi wa Taifa hili,waweze kuliongoza
taifa kwa upendo,amani umaoja na mshikamano uliyopo na kujaribi kukemea matendo
ya kiibisili yanapojitokeza.
Askofu alisema hayo wakati wa mahubiri wakati wa Ibada ya
Alhamisi kuu,katika kanisa kuu la jimbo Kuu la Mtakatifu Mathias Mulumba
Kalemba Manjispaa ya Songea leo.
No comments:
Post a Comment