Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Dkt Norbet Mtega akitoa baraka Jana
KATIKA Ibada ya Ijumaa kuu iliyoanyika katika kanisa la
Jimbo kuu la Mtakatiu Mathias Mulumba Kalemba la Mjini Songea,ambapo waumini wa
Romani Katoliki waliungana na wenzao Duniani Kote,kukumbuka siku ambayo Yesu
Kristu alipotiwa mikononi kwa Ibilisi na kusulubiwa na kufa kwa mateso makali na kufufuka siku ya tatu.
Askofu Mkuu wa Jimbo hilo
Dkt.Norbet Mtega alisema katika mahubiri yake,kuwa Taifa la Tanzania lisichanganye masuala ya kidini na
kiyasiasa,kwa kufanya hivyo haki haitatendeka kwa jamii ya taifa hilo.
Dkt .Mtega alisema kuwa viongozi wa dini zote wawahubiliea
waumini wao maadili mema ya upendo na
amani baina ya dini zenyewe kwa zenyewe na dini nyingine, Serikali iwasaidie
kuhamasisha amani na upendo kwa dini zote,kwa kufanya hivyo hakuna dini itakayo
kuwa juu ya dini nyingine.kwa kuwa wote tuna mwamini Mungu Mmoja.
Aidha alisema Madaraka yatolewe kwa kufuata Katiba ya
nchi,na yasitolewe kwa kufuata kuelewana,udugu,urafiki,ujomba kwa kufanya hivyo
wananchi hawatatendewa haki,unyonge utazidi endelea kwa wale wasiyo kuwa na
ndugu katika ofisi hizo.
Alisema Pasaka hii ni ya mwaka wa Imani kwa Kanisa,kwa hiyo
waumini katika Pasaka hii waliombee taifa hili amani na upendo.Wafanye maombi
kwa ajili ya viongozi wanchi na watu wake.
No comments:
Post a Comment