Sunday, March 31, 2013

BAADA YA PASAKA NILIPATA STAFUTAHI SAFI HAPA NYUMBANI SONGEA

HIVI Ndivyo ilivyo PASAKA hii hapa lwangu.

WAENDESHA BAISKELI WAWE MAKINI WANAPOINGIA BARABARA KUU,ILI KUEPUSHA AJALI KAMA MWENDESHA BAISKELI ALIVYO GONGWA NA PIKIPIKI LEO MJINI SONGEA BAADA YA IBADA YA PASAKA

 Mwendesha baiskeli aliyegongwa na pikipiki leo Mjini Songea
Baadhi ya watu waliyomsogeza mwendesha baiskeli huyo
Mjini kusitokee kitu watu hujaa kushudia tukio.


AJALI ya baiskeli kugongwa na pikipiki katika makutano ya barabara ya Sovi,Polisi katika Manispaa ya Songea iliyotokea leo baada ya mwendesha baiskkeli huyo kuingia barabara kuu bila kusimama na kuangalia pande zote hatimaye kugongwa na pikipiki iliyotokea kona ya Sovi.
Baada ya mwendesha pikipiki kumgonga mendesha baiskeli huyo ambaye jina lake halikutambulika mara moja,wote walianguka kila mmoja na wakati wake.
Mendesha pikipiki alitaka kukimbia,lakini wasamaliam wema walimsihi aende polisi kuelezea tukio hilo,ambapo mwendesha baiskeli alipoambiwa kupelekwa hospitali kwa matibabu alikataa kwa kuogopa hatia kutokana na kuvunja sheria za usalama barabarani.
Kwa hiyo siku kama hizi za sikukuu,watu wanatakiwa kuwa makini katika uendeshaji wa vyombo vya moto na baiskeli kuwa maakini.

IBADA YA PASAKA ILIANZA KWA MAANDAMANO NJE YA KANISA FUATILIA

 Maandamano kabla ya Ibada ya PASAKA,ambapo katika ibada hiyo Askofu Norbert Mtega Kawaombea  Marehemu waliyopoteza maisha yao katika ajali ya kuporomoka kwa jengo la Ghorofa 16 Jijini Dar es Salaam,na majeruhi wapate nafuu ili waweze kujumuika na familia zao.
 Maandamaoni ya akina baba
 Maandamano ya akina mama
 Maandamano ya akina Baba
 Kwaya ya Donbosco
Kwaya ya Donbosco
 Maandamano Askofu Mkuu Norbert Mtega
Maandamano

TANZANIA HAINA HISTORIA YA UMWAGAJI WA DAMU KWA RAIA WAKE HATA WAKATI WA KUDAI UHURU WAKE , ILA SASA TUNAONA DALILI ZA UMWAGAJI WA DAMU KWA BAADHI YA RAIA WAKE.

 Askofu Mkuu Dkt Norbert Mtega akibariki waumini baada ya Ibada ya PASAKA Kanisa kuu la Songea leo.
Waumini wakiwa katika Ibada ya PASAKA
 Waumini
 Kwaya ya DONBOSCO ambayo imekoleza ibada hiyo leo siku ya PASAKA
 Zifuatazo ni picha za umoja wa Wanamama Katoliki ( WAWATA) ,Wa Jimbo la Songea
 Kutoa vipaji akina mama ( WAWATA)

 Vipaji akina mama ( WAWATA )
Katika masomo ya Ibada ya PASAKA akina mama wa WAWATA wakipeleka Biblia ili kwenda kusoma na baadaye Injili.Aliyeshika Biblia menye gauni la kijani ni Bi. Cosensa Mbena na wa pili ni Bi Geni.

KATIKA Ibada ya PASAKA kwenye kanisa kuu la  Katholiki la Jimbo kuu la Songea la Mt.Mathias Mulumba Kalemba mjini Songea,ambao waumini wa kanisa hilo waliungana na wenzao Duniani kote kwa sherehe za PASAKA,
Hata hivyo alisema kuwa nchi ya Tanzania haikuwa na Historia ya umwagaji wa damu hata wakati wa kudai Uhuru wake,lakini kuna baadhi ya raia wamemwaga damu kutoka kwa watu wasio eleweka.
Hayo yametolewa katika mahubiri ya Askofu Mkuu wa Jimbo hilo,Dkt.Norbert Mtega katika Ibada ya sherehe za PASAKA leo,na kwamba ukombozi wa Yesu Kristu kwa kufa na kufufuka kwake uwe kwa watu wote wanao mwamini Mungu hata kama hawajabatizwa.
Aliwashukuru sana waandishi wa habari katika mchango wao wa kuandika na kuripoti uharibifu na vifo kadhaa vilivyo jitokeza katika nchi yetu na wengine  kupata vilema vya kudumu kama vile kutolewa macho.
Alisema kuwa waumini waende kumtangaza ufufuko wake wa  amani,upendo na mshikamano,bila ya kujali tofauti za Imani miongoni mwao,kwani wote ni wana wa Mungu.
Aidha alisema kuwa waumini wanatakiwa kuwa na Biblia mikononi mwao,nyumbani kwao na msalaba ambao ni ukombozi wao,kwani Biblia ni neon la Mungu la uzima ,nasio kama vitabu vingine.na kwamba wanawake wameonekana kuwa na mwamko wa kuwa na Biblia na kushiriki katika Jumuia ndogondogo.

Amewataka wanaume nao kushiriki katika uinjilishaji kwa kwenda kwenye Jumuiya ndogondogo ,pamoja na Biblia kama wanavyo fanya wanawake,ambapo Umoja wa Wanawake katoliki ( WAWATA ) Jimbo la Songea walitoa vipaji katiba Ibada ya PASAKA.

Friday, March 29, 2013

TAIFA LIMETAKIWA LISICHANGANYE MASUALA YA KIDINI NA KISIASA

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Dkt Norbet Mtega akitoa baraka Jana



KATIKA Ibada ya Ijumaa kuu iliyoanyika katika kanisa la Jimbo kuu la Mtakatiu Mathias Mulumba Kalemba la Mjini Songea,ambapo waumini wa Romani Katoliki waliungana na wenzao Duniani Kote,kukumbuka siku ambayo Yesu Kristu alipotiwa mikononi kwa Ibilisi na kusulubiwa na kufa kwa mateso makali  na kufufuka siku ya tatu.

Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Dkt.Norbet Mtega alisema katika mahubiri yake,kuwa Taifa la Tanzania lisichanganye masuala ya kidini na kiyasiasa,kwa kufanya hivyo haki haitatendeka kwa jamii ya taifa hilo.

Dkt .Mtega alisema kuwa viongozi wa dini zote wawahubiliea waumini wao maadili mema ya upendo  na amani baina ya dini zenyewe kwa zenyewe na dini nyingine, Serikali iwasaidie kuhamasisha amani na upendo kwa dini zote,kwa kufanya hivyo hakuna dini itakayo kuwa juu ya dini nyingine.kwa kuwa wote tuna mwamini Mungu Mmoja.

Aidha alisema Madaraka yatolewe kwa kufuata Katiba ya nchi,na yasitolewe kwa kufuata kuelewana,udugu,urafiki,ujomba kwa kufanya hivyo wananchi hawatatendewa haki,unyonge utazidi endelea kwa wale wasiyo kuwa na ndugu katika ofisi hizo.

Alisema Pasaka hii ni ya mwaka wa Imani kwa Kanisa,kwa hiyo waumini katika Pasaka hii waliombee taifa hili amani na upendo.Wafanye maombi kwa ajili ya viongozi wanchi na watu wake.

Thursday, March 28, 2013

IBILISI A ANA NJIA ZAKE ZA KULISAMBALATISHA TAIFA LA TANZANIA

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Norbet Mega Kwenye ibada ya Pasaka
 Askofu Mtega akianzaIbada ya Alhamisi Kuu leo Mjini Songea
 Askofu Mkuu Norbet Mtega akiwa Altareni
 Askofu Mtega akitoa baraka
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Songea Dkt Norbet Mtega akipokea vipaji siku ya Alhamisi kuu.

Mishumaa
 
 


ASKOFU Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbet Mtega amelitahadhahaisha Taifa kuwa Ibilisi wamaingia nchini ili kulisambalatisha taifa ambalo lina amani na ushirikiano wa wakazi ambao wanashirikiana kwa kila jambo kutokana na mshikamano waliokuwa nao.
Askofu Mtega alisema Ibili ana njia nyingi za kulisambalatisha taifa hilo,kwani mambo yamekuwa yanazidi ya kutishia waumini wa madhehebu wa Dini ya Kikristo waogope kwenda kuabudu kwenye nyumba za Ibada kwa ajili ya kumwogopa  ibilisi ailiyoingia nchini.
Alisema Ibilisi hawafurahii,Uhuru,Muungano,Ushirikiano na umoja tuliokuwa nao, bali wanataka kuturudisha katika utumwa, na kila mmoja anaelewa athari za utumwa, hivyo utumwa huo unataka kurudi kama si wao ni watoto wao au wajukuu wao.
Aidha alisema kuwa sumu inayoingia katika taifa kwa kupitia ibilisi, ni adui wa Uhuru wetu,Muungano wetu,Ushirikiano wetu na mshikamano wetu ambapo Wakristu na Waislamu walikuwa akishirikiana katika shida na raha sasa Ibilisi anatumia njia zake kuusambaratisha umoja uliopo.
Alisema tuwaombee viongozi wa Taifa hili,waweze kuliongoza taifa kwa upendo,amani umaoja na mshikamano uliyopo na kujaribi kukemea matendo ya kiibisili yanapojitokeza.

Askofu alisema hayo wakati wa mahubiri wakati wa Ibada ya Alhamisi kuu,katika kanisa kuu la jimbo Kuu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba Manjispaa ya Songea leo.
 

Sunday, March 24, 2013

SIKUU YA MATAWI NI MWANZO WA WIKI YA MATESO YA YESU KRISTO ,LEO WAUMINI KATIKA KANISA LA JIMBO KUU LA SONGEA WAKIWA NA MATAWI WAKISHANGILA,WAKIIMBA HOSANA JUU MBINGUNI.

 Ndani ya kanisa kuu la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba Mjini Songea wakishangilia kwa matawi,Jumapili ya Matawi wakuingana na waumini wengine Duniani kuadhimisha sikuu ya matawi.
 Reverent Father Otieni wa katikati aliyoendesha ibada hiyo takatifu,Pia ni Paroko msaidizi,akisubili vipaji.
 Waumini na mitende yao mikononi
 Waumini wa Jumuiya ya Mfaranyaki wakipeleka vipaji,Anayetoka ni Bwana Matembo fundi hodari wa saa. Mjini Songea.
 Wasichana wa sekondari ya wasichana Songea wakipeleka vipaji vyao

Wakipeleka vipaji

NI mwanzo wa juma kuu la mateso na kusulubishwa msalabani na siku ya tatu akafufuka.Mateso na kufa kwake msalabani ni kwa ajili ya ukombozi wa mwanadamu kwa dhambi zake. Kanisa linakaribia katika adhimisho la Juma la Pasaka Kabla ya Misa kulikuwa na maandamano ikiwa ni ukumbusho wa kuingia kwake Kristu kwa shangwe katika mji wa yerusalemu.Ambapo alipofika mlima ya mizeituni Yesu aliagiza wanafunzi wake wamletee mwana punda .Punda na mnyama mpole,pamoja na upole wake ,punda hutumiwa na watu maskini.ndiyo maana Yesu Kristu alipanda mwana Punda ili kuonyesha kujishusha kwa kupanda punda.Angewza kupanda farasi ambaye hutumiwa na watu maarufu na matajiri ila Bwana alijishusha na kupanda  mwana – punda.
Kwa hiyo kifo  na ufufuo wa Yesu Kristu kwa ajili yetu sisi  kunakofanywa  na umauti wa watu.Na iwapo watu  wakimsadiki yeye watapata uzima wa milele.Wamwaminiye na kumsadiki ambao  wamtangazae na kumuhubiri yeye , watakuwa wanamtangaza na kuihubili Injili kwa watu wote waliyokwisha kata tama ya maisha ya uzima wa milele   hivyo kwa kupitia kwao wataokolewa kwa jina la Yesu
Aidha  waumini wa kanisa hilo kote duniani wamefanya maandamano na matawi mikononi na kuimba Hosana,Mwana wa Daudi,ndiye mbarikiwa,yeye ajae kwa jina la Bwana,Mfalme wa Israeli ,Hosana juu mbinguni.

Wednesday, March 20, 2013

MATAPELI WASICHAFUE DINI ZA WATU KUIBIA WATU FEDHA ZAO,WEZI WA MOROGORO SASA WAMEHAMIA SONGEA WANAJIFANYA WACHUNGAJI AU MAPADRI WANAONUNUA MADINI

KIKUNDI cha matapeli wa Manispaa ya Morogoro wanaojifanya wanaulizia STAMICO na kisha wanajifanya wana  madini aina ya dhahabu ambayo ni dhahabu feki ni koki za maji za shaba zilizoyeyushwa na kuhifadhiwa kwenye vyupa vidogo,sasa wameingia Manispaa ya Songea.
Katika hali siyo ya kutegemea Mama mmoja mkazi wa manispaa ya Songea alikutana na dhahama hiyo,ambapo matapeli hao walimteka hadi Mkoani Njombe,ambako walimtaka Mama huyo akawape fedha milioni 50,ili wampe dhahabu ,Lakini dhambi mara nyingi huwa hazipenyi kwa mtu ambaye amatakasika .Matapeli walivyofika Njombe CRDB Benki walimwamuru mama yule akawachukulie fedha .

Mama alipokaribia mlango wa Benki alizinduka akapata akili ya kupiga simu Songea,matapeli walianza kumkaripia kuwa usiwasiliane na watu maana ni siri yetu wewe na sisi sasa unafanya nini,Roho ya amani ilimjia akaingia Benki ,peke yake,Tapeli wale walitawanyika hawakumfuata ndani ya Benki maana walijua dili imeharibika ,waliingia kwenye gari lao la kifahari.wakakimbia.

Uongozi wa CRDB Njombe ukawasiliana na polisi ambao walimchukua mama huyo na gari la polisi hadi Songea,kati ya  matapeli hao wanne mmoja alijifanya padre yeye ndiye mnunuzi wa madini kumbe tapeli.Kwanini hawa wanachafua Dini za watu kwa  kwa kujifanya mapadre ama wachungaji kwa ajili ya kuibia watu fedha zao? Habari ndiyo hiyo.

Tuesday, March 19, 2013

DKT JAKAYA KIKWETE AMESEMA UFUMBUZI WA UHABA WA MADAKTARI NCHINI NI KUWA NA VYUO VYA KUTOSHA VITAKAVYO TOA WAGANGA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema ufumbuzi wa uhaba wa madaktari nchi ni pamoja na kuwapata wanafunzi wanao maliza mafunzo yao katika vyuo vikuu tulivyo navyo na kujenga vyuo vingine vya fani hiyo.Alisema hayo Jijini Dar es Salaam.

PAPA FRANCIS WA KWANZA AAMESIKIKWA KUSHIKA NAFASI HIYO YA KUONGOZA MAKANISA DUNIANI

 Baba mtakatifu Francis wa kwanza akisoma misa katika viwanja vya Saint Peter's Square Vatican City kabla ya kusimikwa kuwa Papa na kukubali kuliongoza kanisa Katoliki kwa nguvu zake zote Duniani.
 Papa Francis wakati wa mageuzi ya mkate na Divai wakati wa Ibada hiyo Takatifu.
Awali Baba Mtakatifu Francis wa kwanza  katika mahubiri yake amehimiza waumini kufanya maombi ya msamaha wa dhambi.Alisema Mungu hachoki kuwasamehe wanadamu makosa yao,pia amewashukuru waumini wa Kanisa hilo kwa maombi yao kwa sala ya kumuombea Papa Francis wa kwanza.

Thursday, March 14, 2013

KIKUNDI CHA SANAA CHA FATAKI NI MUHIMU SANA KATIKA JAMII YETU

Kikundi cha Fataki kinacho rushwa na TBC, ni kikundi muhimu sana kwa kuielimisha  na kuikosoa Jamii.,Ukipata muda kama upo Tanzania Kifuatilie,hasa wanafunzi wanaochukua Lugha ya Kiswahili.
 Wahenga walisema kuwa hata njinga huwa anatoa wazo litakalo msaidia mjanja.
 Wengi wetu tunazema ni mchezo wa kuigiza,hata kama ni wa kuigiza,je ujumbe wake ukoje kwa Jamii ya Kitanzania? Maadili yamemomonyoka miongoni mwa vijana, haiyamkini hata watu wazima ambao wanaiga mambo bila ya kuchuja madhara yake kwa Jamii.


Kikundi cha sanaa cha Fataki ambacho kinarushwa na TBC kina umuhimu mkubwa kwa jamii yetu ya Tanzania hasa wakati huu ambao jamii inashangaa kuona vikundi vinavyoibuka kila kukicha vinafanya mambo ambayo Jamii yetu ya Kitanzania  na Kiafirika haijawahi kufanya.

Kikundi hiki nasema ni muhimu kwakuwa ,wanaikosoa,wanaelimisha,wanaitahadharisha na wanaiburudhisha Jamii kwa kupitia Fasihi Simulizi,ambamo ndani yake kuna Maudhui,Ujumbe,Fasihi,Misemo,Methali pamoja na Vivumishi,ambavyo Mwanafasihi akikifuatikila kipindi hicho anaweza akaandika kitabu cha fasihi  ambayo itasaidia kwenye kukuza Lugha yetu ya Kiswahili.

Hasa vijana wanaosoma wangejaribu kukifuatilia kipindi hicho kinachorushwa na TBC, ninaimani,akirudi kusoma vitabu vya Fasihi ( Fasihi andishi ) hatapata shida kubwa katika kuchambua Fasihi na Kumchambua Mwandishi wa Fasihi hiyo.

Tatizo vijana wetu hawana muda wa kuangalia Tamthilia kama zile,huwenda wakidai wanakikundi taaluma yao ni ndogo,lakini tukumbuke Lugha haina elimu, elimu itaongezeka ukienda shule ambako utaenda kuiboresha ili upate Lugha fasaha.

Pia Fasihi simulizi ilianza kabla hata maandishi hayajaanzwa,ilikuwa kwenye unyago,jando, sherehe na misiba.Ndiyo maana kwenye sherehe nyimbo na ngoma zina pigwa na kuimbwa,hali kadhalika kwenye misiba watu wanaimba nyimbo za kuomboleza na hata kucheza kwa baadhi ya makabila.

Leo nimevutiwa na kikundi hicho pale walipotamba na kumsihi kijana ambaye alishika upanga kwenda kupambana na watu ambao wamechinja ,kwake yeye mnyama aliye chinjwa na watu hao yeye hawezi kula,maana yeye ndiye aliyekabidhiwa kisu kuchinja,lakini wazee walimpa darasa na akaelewa kuwa alicho taka kukifanya hakiipendezeshi Jamii.

 ‘ Babu zetu walikuwa wakichinja lakini kila watu walikuwa wakiabudu vitu ambavyo katika ibada zao wa alikuwa wanajua wanampendezesha Mungu,Dini hizi zimeletwa tu hatukuwa nazo, kwanini tuifukuze Amani nchini kwetu kwa ajili ya Dini zilizoletwa” alisema mzee mmoja.

Wednesday, March 13, 2013

BREAKING NEWS, SAINT PETER'S SQUARE,VATICAN CITY, HIS HOLINESS FRANCIS POPE SECTED

 His Holiness Francis a new Pope,people celebrated after white smoke ,Thank you God to receive power to Cardinals to select a new Pope.
 A new Pope at Saint Peter's Square,Vatican City today,he asked people to pray for him.