Tuesday, April 10, 2012

WAZIRI MKUU KAZINDUA CHUO CHA VETA KONGOWE KIBAHA PWANI

 Waziri Mkuu Mizengo Peter Pinda akiongea na wananchi,uongozi wilaya na mkoa pamoja na wanafunzi kabla ya kuzindua Chuo cha VETA Kongowe Kibaha Pwani.
 Hicho ni chuo cha VETA kilichoko Kongowe aliye mbele ya jengo hilo ni mwandishi wa habari wa ITV
 Mwenyekiti wa Bodi ya VETA akimshukuru mgeni rasmi,na kusema atatekeleza yote yaliyo semwa na Waziri Mkuu.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho cha VETA Kongowe.


WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Mizengo Peter Pinda leo amezindua Chuo Cha VETA Kongowe Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani ambacho kina wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa fani mbalimbali.
Mhe.Pinda alisema chuo hicho ni muhimu sana kwa vijana wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari.kwa hiyo wanafunzi wanaomaliza elimu katika ngazi hizo mkoani Pwani wapewe nafasi ya kwanza ndipo wapatiwe wa kutoka mikoa ya nje nafasi kama zita kuwepo.
Aidha Pinda ameipongeza serikali ya Korea Kusini kwa kutoa fedha na vifaa katika ujenzi wa chuo hicho,  Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  na pia uongozi wa Bodi ya VETA  kwa jitihada zao za kuendesha vyuo hivyo nchini
Mhe. Pinda aliwaambia wanafunzi wa chuo hicho wakitunze,wasianze kupiga mawe kukiwa na maatizo na kama yakitokea waende kuomba ushauri kwenye uongozi wa wilaya,ikishindwa Mkoa na hata  kwa Mbunge wao.

No comments:

Post a Comment