Tuesday, April 17, 2012

RAIS WA VICOBA TANZANIA AZINDUA KAMPENI YA VICOBA JIJINI DAR ES SALAAM MGENI RASMI DKT REGINALD MENGI ACHANGIA SHILINGI MILIONI MIAMOJA

Rais wa VICOBA Mhe.Devota Likokola amesema Dkt Reginald Mengi ni Mtanzania wa pekee mwenye kujali watu  maskini,na mpiganaji mkuu wa umaskini Tanzania,anatumia utajiri wake kwa ajili ya kuinua maisha wa watu wenye kipato cha chini.Alisema Dkt Mengi amechangia VICOBA fedha za kitanzania Tshs.bilioni moja na milioni miamoja na ishirini,kwa ajili ya kuendeleza watu maskini,watu wenye mashaka ya maisha.
Alisema hayo kwenye uzinduzi wa Kampeni ya VICOBA Jijini Dar es Salaam, ambapo Mengi alikuwa mgeni rasmi,uzinduzi uliyoambatana na kupewa vyeti walimu 30 wa VICOBA ambao watakwenda kuhamasisha VICOBA kwenye maeneo yao.
 Dkt Reginald Mengi alisema vita vya kupigana na umasikini si vya mtu mmoja ni vya kila mmoja.Na mwenye kujua uchukungu wa umaskini ni maskini mwenyewe,yeye anaujua umaskini,hivyo ni juu yake kujitoa kwenye umaskini huo.na watu wenye vipato wao ndiyo wa kuwasaidia watokane na  umaskini wa kipato.Amewaomba matajiri kutoa sehemu yao ya utajiri kusaidia watu maskini ili na wao wawe na unafuu wa maisha.Katika uzinduzi huo Dkt Mengi amechangi shilingi milioni miamoja kwa ajili ya walimu wa VICOBA waliyopewa vyeti kwenda kufundisha vikundi vya uzalishaji mali kupitia VICOBA.
 Mwenyekiti wa VICOBA Bibi Monica Mbega alisema kuwa kazi ya wara
tibu wa VICOBA ni ya kujitolea siyo ya kipato ,aidha alisema VICOBA vimeinua sana maisha ya watu wenye kipato cha chini.Pia amempongea Dkt Mengi kwa moyo wake wa kujitoa katika uchangia wa kipato chake kwa ajili ya maskini nchini.Na Rais wa VICOBA kuwa na moyo wa kuanzisha ba kuendeleza VICOBA kwa ajili ya kuinua maisha ya wa - Tanzania wenye kipato cha chini,ikiwa ni jitihada za kupambana na vita vya umaskini.

Baadhi ya wana - VICOBA na walimu waliyo tunukiwa vyeti vya mafunzo ya kuendesha VICOBA katika maeneo yao

No comments:

Post a Comment