Sunday, April 8, 2012

Malori yameanza kupita katika barabara ya Newala Mtwara baada ya kufungwa kwa magogo na wananchi wenye hasira ya kutokulipwa malipo yao ya korosho Tarafa ya Nanyamba

 Barabara ya Newala kwenda Mtwara ilikuwa imefungwa kwa magogo makubwa na wananchi ,wakulima wanaodai malipo ya pili ya zao la korosho Nanyamba mkoani Mtwara.Leo imefunguliwa baada ya uongozi wa wilaya kwenda kuzungumza na wakulima wa zao hilo na kufikia mwafaka wa kutoa magogo hayo barabarani , magari yameanza kupita.
Hao ni baadhi ya wakulima ambao wanalalamikia uongozi wa wilaya kwa kuchalewesha malipo ya pili ya zao la korosho,ambapo madereva wa malori hayo nao wanasema wawo kufungiwa barabara ni kuwakosea haki maana wao hawahusiki na malipo hayo.

No comments:

Post a Comment